IQNA

Jinai za Israel

Shiriki Mkutano wa Kimataifa kuhusu 'Miaka 75 ya Kukaliwa kwa Mabavu Palestina'

15:07 - March 01, 2024
Habari ID: 3478437
IQNA - Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa kinapanga kuandaa kongamano la kimataifa la "Miaka 75 ya kukaliwa kwa mabavu Palestina".

Kituo cha Sayansi ya Kiislamu na Kijamii  chuo kikuu hicho kimetuma ilani ya kupokea makala kwa mujibu wa mada ya mkutano huo.

Kulingana na Seyed Mehdi Taheri, katibu wa kisayansi wa mkutano huo, wale wanaopenda kushiriki  wanaweza kuwasilisha makala zao kwa Kiajemi, Kiingereza, Kiarabu, Kifaransa, Kituruki na Kiurdu.

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha makala itakuwa Mei 10, 2024, alisema, akibainisha kuwa mkutano huo utafanyika Mei 30, 2024.

Vituo na taasisi kumi na sita za kitaaluma na utafiti zitashirikiana na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa katika kuandaa hafla hiyo, alisema.

Taheri amebaini kuwa, maudhui kuu katika kongamano hilo ni pamoja na Misingi ya Kielimu ya Kadhia ya Palestina, Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na Athari Zake, na Mikakati ya Kutatua Kadhia ya Palestina ndio mada kuu za mkutano huo

Mbali na maudhui hizo kuu kutakuwa na maudhui ndogo zinazohusu 'Kukaliwa kwa Mabavu  Palestina kwa Mtazamo wa Sheria', 'Nyaraka na Sheria za Kimataifa', 'Uungaji Mkono kwa watu Wanaodhulumiwa wa Palestina kwa Mtazamo wa Uislamu na Imani Nyingine', 'Wajibu wa Serikali na Jumuiya za Kimataifa Kuhusiana na Utawala wa Israel Kukalia kwa Mabavu Palestine', na 'Utawala wa Kizayuni wa Israel unavyokiuka. haki za binadamu.'

Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo tembelea tovuti ya mkutano hapa.

 

4202507

Habari zinazohusiana
captcha