Kikirejelea matukio ya kusikitisha kama vile watoto kuganda hadi kufa mikononi mwa mama zao na kuharibiwa makazi ya muda, kituo hicho kilitoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kimataifa kushughulikia hali hiyo.
Katika taarifa yake ya Jumamosi, Al-Azhar ilieleza huzuni yake kubwa juu ya "kushindwa kwa jamii ya kimataifa" kushughulikia mateso ya watu wa Palestina huko Gaza.
Ilisema kuwa zaidi ya miezi 15 ya vita na mzingiro imeunda hali mbaya, hasa wakati wa msimu mkali wa baridi.
“Uhalifu dhidi ya Gaza, ikiwa ni pamoja na maangamizi ya kikaumu, mauaji ya kimbari, na mauaji ya halaiki, umesababisha janga kubwa la kibinadamu. Wanawake, watoto, na wazee wanakabiliwa na shida zisizovumilika,” ilisomeka taarifa hiyo.
Kituo hicho kilielezea changamoto maalum zinazowakabili wakazi wa Gaza wakati wa msimu wa baridi, kikisisitiza majanga kama vile watoto kufa kutokana na baridi kali na uharibifu wa makazi.
Al-Azhar ililaani kile ilichoelezea kama kutojali kwa jamii ya kimataifa na kukataa kwa viongozi wa kisiasa kuchukua hatua za kijasiri kumaliza "uchokozi wa jinai wa utawala wa Israel."
Taarifa hiyo ilitoa wito wa "hatua madhubuti na za haraka" kuhakikisha misaada ya kibinadamu inafikia Gaza, ikitoa nafuu kwa wakazi wake waliokabiliwa na shida.
Ilihimiza mashirika ya kimataifa na serikali duniani kote kuchukua hatua kumaliza mzingiro na kupunguza mateso ya Wapalestina, ikisisitiza haki yao ya msingi ya kibinadamu na ulinzi chini ya sheria za kimataifa.
Hii inakuja katikati ya ripoti zinazoendelea za kuongezeka kwa hali mbaya ya maisha huko Gaza, ambapo karibu wakazi wote wa milioni 2.3 wamehamishwa kutokana na vita vya mauaji ya kimbari vilivyoanzishwa na utawala katili wa Israel dhidi ya eneo hilo Oktoba mwaka jana. Tokea wakati huo, jeshi katili la Israel limeua zaidi ya Wapalestina 46,000, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.
3491420