Akizungumza na IQNA, Hujjatul Islam Hamid Shahriari, katibu mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu (WFPIST), ameashiria historia ya eneo la Asia Magharibi, akibainisha jinsi madola ya kikoloni yalivyoibua migawanyika katika nchi za Kiislamu.
Kufuatia vita vya dunia, madola ya kikoloni yalileta mgawanyiko katika ulimwengu wa Kiislamu, kuunda mataifa madogo, kugawanya mataifa, na kuweka mipaka kwa njia ambazo mara nyingi hugawanya makabila ya mipakani, alisema, akiongeza kuwa ukoloni ulichochea migogoro inayoendelea ya mipaka na kudumisha mgawanyiko mkubwa katika mataifa ya Waislamu.
Madola ya kikoloni yakiongozwa na Marekani, yalifanya kazi kikamilifu kupanua mifarakano na migogoro katika eneo hilo, na kufanya mgawanyiko kuwa sera kuu, alisema Shahriari. "Katika karne iliyopita, moja ya hatua zake muhimu zaidi ilikuwa kuanzishwa kwa Israeli kutumia uvimbe huu wa saratani kuwashinikiza watawala wa kikanda."
"Genge la wahalifu limelazimishwa katika eneo letu na mataifa haya yenye nguvu duniani ambayo yameingiza hofu katika eneo, kama ilivyoonekana katika mwaka uliopita, kwa lengo la kutumia mipasuko iliyoko. Hata hivyo, walipuuza uwezekano kwamba jambo hili lingeweza kukuza bila kukusudia hali ya umoja miongoni mwa nchi za Kiislamu,” aliongeza.
Alikuwa akiashiria vita vya mauaji ya kimbari vya Israel dhidi ya Gaza na Lebanon. Utawala wa Israel umekuwa ukivamia eneo lililozingirwa la Ukanda wa Gaza na kusini mwa Lebanon katika mwaka uliopita. Uchokozi wa pande mbili za Israel, unaoungwa mkono na mataifa ya Magharibi, umeua zaidi ya watu 45,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, huko Gaza na Lebanon.
Uchokozi huo ulianza baada ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Wapalestina huko Gaza kuanzisha Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa mnamo Oktoba 7 mwaka jana, ili kukabiliana na miongo kadhaa ya jinai za Israel dhidi ya Wapalestina.
"Kwa maoni yangu, Operesheni ya Al-Aqsa ya mafuriko imesimamisha juhudi za Israel za kuendeleza miradi kama vile Makubaliano ya Ibrahim na mipango mingine ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel ambayo inakinzana na umoja wa Kiislamu," Shahriari alisema, akimaanisha mpango unaoongozwa na Marekani wa kurejesha uhusiano kati ya utawala haramu wa Israel na nchi za Kiislamu.
"Juhudi hizi kimsingi zimeondolewa kwenye ajenda na kusukumwa pembeni, hivyo leo, ni wachache wanaothubutu kuzungumza waziwazi kuhusu uhusiano na utawala unaonyakua wa Kizayuni," aliongeza.
"Wakati huo huo, ushirikiano wa kitaifa na kimadhehebu baina ya nchi za Kiislamu unabadilika na kuwa muungano usiotarajiwa, na kuunda aina ya umoja kati yao," aliongeza, akiashiria hatua ya Saudi Arabia na nchi zingine za Kiarabu na Kiislamu ya kulaani shambulio la hivi karibuni la Israel dhidi ya Iran kama mfano.
Aidha Hujjatul Islam Shahriari ameashiria juhudi za kujenga umoja unaooimarika kati ya Waislamu, na kusema kwamba "Diplomasia ya Umoja inaendelea katika ngazi tatu."
Ngazi ya kwanza ni diplomasia ya umma, alisema. "Tumetumia uwezo wa vyombo vya habari, mtandao, na majukwaa ya kijamii katika ustaarabu wa ulimwengu wa Kiislamu. Tunaamini kwamba kila mtu katika ulimwengu wa Kiislamu anaweza kuwa na sauti ya umoja. Hapo awali hatukiwa na mitandao lakini sasa tuna uwezo huu."
Akitaja ngazi ya pili kama diplomasia ya wanazuoni, Hujjatul Islam Shahriari amesema kwamba wanazuoni wa Shia na Sunni "waliingiliana mara chache" hapo awali kutokana na changamoto mbali mbali. "Leo, vikwazo hivi vimeondoka, na kuongeza uwezekano wa diplomasia ya wanazuoni na maulamaa ili kukuza umoja katika ulimwengu wa Kiislamu."
Ngazi ya tatu ni diplomasia ya kisiasa, amesema, na kuongeza kwamba ukweli kwamba mchakato wa baadhi ya nchi za Kiislamu kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel hauko tena au umesitishwa kwa muda na hayo ni mafanikio makubwa.
Ngazi hizi tatu za diplomasia zimepata maendeleo makubwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kufuatia Operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa, ambapo watu duniani kote wanafahamu zaidi dhulma wanazopata Wapalestina hasa wa Gaza na wanaonyesha mshikamano nao, alisema.
3490474