IQNA

Jinai za Israel

Rais wa Brazil: Utawala wa Israel unatekeleza mauaji ya kimbari Gaza

14:42 - February 24, 2024
Habari ID: 3478407
IQNA-Rais Luiz Inácio Lula da Silva wa Brazil amesema kuwa, kinachofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza ni mauaji ya KIMBARI.

Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, utawala wa Kizayuni unafanya mauaji na jinai kubwa kupindukia dhidi ya Wapalestina hasa wa Ghaza kwa uungaji mkono kamili na wa pande zote wa madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani, Uingereza na Ujerumani. 

Mapema leo Jumamosi, shirika la habari la IRNA limemnukuu Rais wa Brazil akisema kwenye tamko lake kwamba, jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza ni mauaji ya halaiki ya watu wasio na hatia hasa wanawake na watoto wadogo.

Amesema, Wanawake na watoto wadogo wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza wananyimwa haki zao za kimsingi kabisa kama chakula, maji na matibabu huku Israel ikiendelea kuwashamblia kwa mabomu na silaha zilizopigwa marufu, wananchi hao wasio na ulinzi.

Hivi karibuni pia Rais Lula Da Silva wa Brazil aliufananisha utawala wa Kizayauni wa Israel na ule wa Wanazi wa Ujerumani wakati alipohutubia kikao cha 37 cha wakuu wa Umoja wa Afrika AU, mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Utawala wa Kizayuni ulichomwa sana na uhakika huo kutoka kinywani na Rais wa Brazil na ulidai kuwa, Da Silva si mtu anayekaribiwa kwa utawala wa Kizayuni. 

Kufuatia matamshi hayo ya Wazayuni dhidi ya Rais Da Silva, serikali ya Brazil ilimrejesha nyumbani balozi wake aliyekuwa anaiwakilisha nchi hiyo kwa utawala wa Kizayuni na hadi leo inaendelea kusimama imara kuwaunga mkono wananchi wanaoteseka kila upande wa Ukanda wa Ghaza na maeneo mengine ya Palestina.

3487315

captcha