IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Tovuti ya idhini ya vibali vya futari katika Msikiti wa Makka yazinduliwa

20:25 - March 05, 2024
Habari ID: 3478455
IQNA - Tovuti ya kielektroniki imezinduliwa nchini Saudi Arabia ambapo watu wanaweza kuomba vibali vya kula futari kwa makundi kwenye Msikiti Mkuu wa Makaa

Tovutib hiyo inalenga kurahisisha mchakato wa kutuma maombi kwa wale wanaotaka kuandaa  futari kwa makundi katika mwezi mtukufu wa Ramadhan katika eneo hilo takatifu..

Kwa mujibu wa taarifa ya Arab News, tovuti hiyo imezinduliwa na Mamlaka Kuu ya Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu yaani Haramein nchini Saudia..

Kumpa chakula cha iftar Mwislamu mwenye kufunga saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani inachukuliwa kuwa ni amali njema katika Uislamu na inahimizwa, na hii ndiyo sababu Waislamu wana shauku ya kukaribishana wakati wa Ramadhani na kubadilishana zawadi za chakula.

Mwezi wa Ramadhani (ambao huenda ikaanza Machi 12 mwaka huu) ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu.

Ni kipindi cha sala, saumu, utoaji wa sadaka na uwajibikaji kwa Waislamu duniani kote.

Wakati wa Ramadhani, Waislamu hufunga (kujiepusha na vyakula na vinywaji) kuanzia wakati wa kabla ya Sala ya Afajiri hadi Magharibi.

3487421

captcha