IQNA

Ramadhani

Maqari wa Iran na Kuwait wasoma Qur'ani kwa mtindo wa Munafisah katika Kipindi cha TV cha Mahfel (+Video)

6:14 - April 08, 2024
Habari ID: 3478651
IQNA - Qari wa Iran Ustadh Hamed Shakernejad na Qari wa Kuwait Sheikh Abdullah Abul Hassan wamesoma Qur'ani kwa mtindo wa Munafisah katika kipindi maarufu cha televisheni cha Qur'ani nchini Iran kinachojulikana kama Mahfel.

Munafisah maana yake ni kupokezana kusoma aya za Qur'ani Tukufu. Qari mashuhuri wa Kuwait alisoma Aya za 117 na 118 za Surah Al-Muminun na kisha Aya 1-6 za Surah Al-Balad. Usomaji wake ulifuatiwa na usomaji wa Ustadh Shakernejad.

Walisoma Munafisah katika msimu wa pili wa Mahfel, kipindi cha Televisheni cha Qur'ani kinachorushwa hewani na kanali ya tatu ya televisheni ya Shirika la Utangazaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mahfel ni kipindi maalum cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Onyesho la msimu wa pili wa kipindi hicho maarufu lilianza kwenye chaneli ya 3 ya IRIB  katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mnamo Machi 12.

Kipindi hicho hutangazwa kabla ya Magharibi kila siku katika mwezi mtukufu, na kuwapa watazamaji hali nzuri ya kiroho wanapojitayarisha kufuturu.

Kwa kuzingatia Qur'ani, kindi hiki kinalenga kuwapa watu waliofunga muda mfupi wa kunufaika na  mijadala yenye utambuzi na usomaji wenye kuvutia wa Qur'ani Tukufu.

4209230

captcha