IQNA

Watetezi wa Palestina

Mjukuu wa Mandela asema jinai za kivita za Israel  zilianza muda mrefu kabla ya Oktoba 2023

21:14 - May 28, 2024
Habari ID: 3478898
IQNA - Mjukuu wa mwanasiasa shujaa aliyepinga ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini Nelson Mandela amesisitiza kwamba mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina yanayotekelezwa na Israel hayakuanza Oktoba 7, 2023 baada ya Operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa.

Nkosi Zwelivelile Mandela alisema jinai za "mauaji ya halaiki, mauaji ya kikabila, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu" nchini Palestina zimekuwa zikiendelea kwa miaka 76.

"Vita havijatokea tangu tarehe saba Oktoba, lazima tuwe wazi juu ya ukweli ni upi. Mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita wa maangamizi ya kikabila, na uhalifu dhidi ya ubinadamu ni jinai ambazo  zimekuwa zikiendelea kwa miaka 76 iliyopita tangu 1948,” alisema mjumbe wa huo wa Bunge la Afrika Kusini katika mahojiano na Anadolu mjini Geneva.

Mandela aliongeza kuwa zaidi ya vijiji 531  vya Wapalestina vimeangamizwa  na utawala Kizayuni.

Amesisitiza kwamba kumekuwa na zaidi ya mauaji 20 tofauti kati ya 2006 hadi 2023 huko Gaza pekee, alisema mengi zaidi yametekelezwa katika maeneo yanayokaliwa katika Ukingo wa Magharibi.

"Tunalaani vikali ukweli kwamba watu kila mara walitaka kuzungumza kuhusu mzozo huu kana kwamba ulianza tarehe saba Oktoba," alisema.

Akizikosoa serikali ambazo si "sauti za watu wengi", alisema watu wanaongezeka katika kila mji mkubwa duniani kote kuunga mkono kadhia ya Palestina.

"Intifada ya Kielektroniki imeweza kutumia mitandao ya kijamii na kuhakikisha kwamba tunaweza kufikia mbali na kote katika jumuiya ya kimataifa na kuhamasisha uungaji mkono kwa watu wa Palestina," aliongeza.

Akisifu juhudi za serikali yake na rais, alisema yamekuwa "mafanikio ya kihistoria" kwa upande wa Afrika Kusini.

Mandela alitoa "wito wa kimataifa" kwa nchi zote za Ulaya, Magharibi, na Amerika ya Kusini, Afrika, na Asia, akizitaka kufuata na kuunga mkono kesi ya Afrika Kusini.

"Tunafurahi sana kusikia kwamba Uhispania na nchi zingine sasa zimeitambua Palestina kama taifa, na tutaendelea kutoa wito kwa nchi zaidi kufuata vivyo hivyo," aliongeza.

Afrika Kusini ilikuwa nchi ya kwanza kuwasilisha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala huo Gaza kuanzia Oktoba 7. Tokea wakati huo utawala katili wa Israel umeua zaidi ya Wapalestina 36,000 wengi wakiwa ni wanawake na watoto na kujeruhi wengine wasiopungua 80,000. Aidha inaaminika Wapalestina zaidi ya 10,000 wamezikwa chini ya vifusi kote Gaza.

3488523

Habari zinazohusiana
Kishikizo: mandla mandela gaza
captcha