IQNA

Shughuli za Qur'ani Tukufu Misri

Mashindano ya Qur'ani, tarjuma za Qur'ani ni miongoni mwa shughuli kuu za Wizara ya Wakfu Misri

11:32 - December 30, 2022
Habari ID: 3476329
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Wakfu ya Misri katika ripoti iliangazia shughuli zake mwaka 2022, na kusema kuandaa mashindano ya kitaifa na ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kuwa miongoni mwa kazi muhimu zaidi ilizofanya.

Wizara hiyo ilisema katika ripoti hiyo kwamba, imefanya juhudi kubwa mwaka 2022 kwa lengo la kukuza fikra za mitazamo ya wastani katika Uislamu na kurekebisha sintofahamu na imani potofu kuhusu Waislamu katika ngazi ya kimataifa.

Wizara hiyo imesema iliandaa mashindano mbalimbali ya Qur'ani katika ngazi tofauti za ndani, kitaifa na kimataifa, yakiwemo ya wanafunzi wa kigeni wanaoishi Misri.

Wizara ya Awqaf pia ilituma zaidi ya viongozi 100 wa maombi na waenezaji kwa nchi tofauti za Asia, Afrika, Ulaya na Amerika Kaskazini na Kusini mwaka 2022.

Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, wasomi 62 wa Kiislamu walitumwa katika nchi 20 kwa ajili ya kuhubiri, ripoti hiyo iliongeza.

Kutarjumina kuchapisha tarjumai tatu za Qur'ani Tukufu- katika Kigiriki, Kihausa, na Kiebrania, na uchapishaji wa vitabu 95 kuhusu masuala mbalimbali ya kidini ni miongoni mwa shughuli nyingine za huduma.

Pia iliandaa programu nyingi za kidini na Qur'ani katika zaidi ya misikiti 6,000 kwa ajili ya wananchi wakiwemo watoto na vijana, ripoti hiyo iliongeza.

Ripoti hiyo iliendelea kusema kuwa mwaka 2022, wizara ilitoa zawadi ya vitabu vya dini na Kiislamu kwa mashirika na vituo vya Kiislamu katika nchi mbalimbali kama vile Ghana, Austria, Marekani, Uswisi, Uzbekistan, Venezuela, Ujerumani, Italia, Malaysia, Kuwait, Hispania, Mauritania, Indonesia na Tanzania.

Nchini Misri, Wizara ya Wakfu ina jukumu la kuandaa, kuratibu na kusimamia shughuli za Qur'ani na kidini.

4110216

captcha