Lengo la tatu ambalo Imam Hussein (AS) analitaja kwa uasi wake ni “kufanya kwa mujibu wa Siira na Sunna za babu yangu na njia ya baba yangu Ali ibn Abi Talib (AS).”
Katika Fiqh ya Kiislamu, Siira ya Mtukufu Mtume (SAW) na Qur'ani Tukufu ni vyanzo viwili vikuu vya kupata hukumu za kidini.
Mwenyezi Mungu anasema katika aya nyingi za Qur’ani Tukufu kwamba pamoja na utii kwa Mwenyezi Mungu, kumtii Mtume (SAW) na Ulul Amr pia ni Wajib.
Kwa mfano, katika Aya ya 59 ya Surah An-Nisa tunasoma: “Enyi mlio amini!
Aya inaendelea kusema: “Ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Kiyama, basi rejeeni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika mambo mnayo khitalifiana. Hii itakuwa njia nzuri zaidi na bora ya kutatua tofauti.
Kwa hivyo kurejelea Siira ya Mtukufu Mtume (SAW) ni amri ya Qur'an na inapotokea masuala ambayo yanasababisha migogoro katika jamii, suluhu iko katika kurejelea Siera ya Mtume (SAW).
Mtume (s.a.w) alisimama dhidi ya Mushrikeen (washirikina) na kamwe hakukubali vitisho vyao au kuvutiwa na ahadi zao.
Hata aliingia vitani na Mushrikeen ili wasiweze kuzuia kuenea kwa Uislamu na kuwaongoza watu kwenye njia iliyonyooka.
Kuamrisha Mema, Kukataza Maovu Lengo la mauaji ya Imam Hussein (AS)
Kwa mujibu wa Hadith, Mtume (s.a.w) alisema Jihad bora ni neno la ukweli lililosemwa mbele ya mtawala dhalimu.
Na hivi ndivyo alivyofanya Imam Hussein (AS); Alipoona kuwa mtu fisadi kama Yazid ibn Muawiyah ameingia madarakani na kutaka kuchukua hatua zitakazopelekea kuutokomeza Uislamu wa kweli, Imam Hussein (AS) hakunyenyekea kwake bali alizungumza kwa uwazi kabisa neno la ukweli mbele ya watu, Yazid na mamluki wake.