IQNA

Mtazamo

Mwanazuoni: Katiba ya Madina inaweza kuigwa katika majadiliano baina ya dini mbalimbali

16:48 - October 28, 2024
Habari ID: 3479660
IQNA – Mwanazuoni mmoja amesitiza kuwa Katiba ya Madina, iliyoanzishwa na Mtume Muhammad (SAW), inaweza kuwa kielelezo muhimu cha mazungumzo ya kisasa baina ya dini mbalimbali.

Hujjatul Islam Taher Amini Golestani, mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Amani na Dini, amesisitiza haja ya mazungumzo kati ya jumuiya za kidini kama msingi wa kuishi pamoja kwa amani.
Akizungumza siku ya Jumapili kwenye semina ya kukuza utangamano miongoni mwa wafuasi wa dini na madhehebu mbalimbali, alibainisha historia ya mazungumzo kati ya dini mbalimbali.
"Tangu miaka ya 1960, Vatikani imesimamia mazungumzo kama jibu la mizozo ya karne nyingi, ikitetea majadiliano kama hatua muhimu. Ifahamike kuwa Mtume Muhammad (SAW) pia alisisitiza kuhusu mazungumzo katika barua kwa Wakristo, ambayo inaonekana muhimu sana leo," amesema Golesatani.
AIdha ameelezea mageuzi ya mijadala ya dini mbalimbali kupitia awamu nyingi. "Mazungumzo hapo awali yalilenga kuwageuza wengine au kupinga imani zao," alieleza. "Baada ya muda, ilibadilika ili kukuza uelewa wa kitamaduni, kutambua uwezo wa pande husika, na hatimaye kujadili maadili ya pamoja. Hata hivyo, hatua ya sasa ni fursa ya kipekee ya kutambua ufumbuzi kwa changamoto za pamoja."
Alipendekeza kuwa sasa ni wakati wa kushirikiana katika kutatua matatizo yaliyopo baina ya wafuasi wa dini mbali mbali . "Kwa maoni yangu, Katiba ya Madina, iliyoasisiwa na Mtume Muhammad (SAW) kama katiba ya kwanza ya dunia, ni marejeo muhimu," aliongeza.
"Kabla ya Muhammad kuwa Mtume, Waarabu na Wakristo walikuwa mara kwa mara katika vita. Katiba hiyo ilikusudiwa kuwaunganisha watu kwa misingi ya ubinadamu."
Golestani aliangazia umuhimu wa waraka huu, akiuelezea kama mfano wa kidiplomasia na mikakati mingi ya kuzuia vurugu miongoni mwa wafuasi wa dini tofauti. "Barua ya Mtume (SAW) kwa Wakristo pia inaweza kuwa mfano."
Golestani amewataka viongozi wa kidini kuelekeza mijadala katika utatuzi wa matatizo, kwa kutumia mifumo iliyopo ya kisheria ya kimataifa. "Viongozi wa kidini mara nyingi hawana ujuzi wa rasilimali hizi za kisheria, ambazo zinaweza kusaidia juhudi zao za kuleta mabadiliko chanya."

4244712

Habari zinazohusiana
captcha