Hafla ya kuinua bendera ilihudhuriwa na viongozi wa kidini, kisiasa na kijamii, msomi na wanafunzi wa seminari, watu wa vyuo vikuu na idadi kubwa ya mahujaji.
Ahemd al-Qureishi, afisa wa Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Ali (AS) alihutubia katika hafla hiyo, akitoa salamu za rambirambi katika tukio hilo la majonzi na kuzungumzia vipengele tofauti vya kufariki kwa Mtukufu Mtume (SAW).
Hapo awali mamlaka ya Najaf ilisema kuwa kutokana na idadi kubwa ya wafanyaziara wanaotarajiwa kuzuru eneo takatifu siku hizi, wanajeshi na vikosi vya usalama vimeongeza hatua ili kuhakikisha usalama.
Siku ya 28 ya mwezi wa Hijri wa Safar, ambayo inaangukia Jumatatu, Septemba 2, ni kumbukumbu ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (SAW) na kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hassan (AS).
Siku ya 30 ya mwezi wa mwandamo, Septemba 4 mwaka huu, inaadhimishwa kama kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Ridha (AS), Imam wa nane wa Shia.
3489740