Tarehe 28 Safar, liyoangukia Jumatatu, Septemba 2 mwaka huu, ni kumbukumbu ya kufariki dunia Mtume Mtukufu Muhammad (SAW) na mwaka wa kuuawa shahidi Imam Hassan Mujtaba (AS).
Haidar Rahim, mkuu wa kituo cha uenezaji habari cha idara hiyo, alisema wafanyaziara na waombolezaji milioni 5 walitembelea kaburi hilo takatifu siku ya Jumatatu.
Alisema Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Ali (AS) na taasisi na mashirika mengine yalifanya juhudi za kila njia kuwezesha kuwasili kwa wafanyazaiara na kuwahudumia.
Wakati huo huo, gavana wa Najaf, Yousef Makki kanawi, alipongeza mafanikio ya mpango wa usalama uliowekwa wa tarehe 28 Safar.
Pia, kamati kuu ya usalama ilisema kwamba idadi ya mahujaji mwaka huu ilizidi ile ya miaka iliyopita.
Licha ya idadi kubwa ya wafanyazaiara, hakuna matukio ya kiusalama yaliyoripotiwa wakati wa ibada za maombolezo zilizofanyika kwa kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (SAW) na kumbukumbu ya kifo cha kishahidi cha Imam Hassan (AS), iliongeza .
3489750