IQNA - Mawkib yenye jina la "Neda al-Aqsa" (Wito wa Al Aqsa) imeundwa kwenye nguzo nambari 833 ya barabara ya Najaf-Karbala nchini Iraq katika matembezi ya Arbaeen ya mwaka huu. Mawkiba hii inakaribisha wafanyaziara na maafisa ambao husimama ili kutoa sauti zao za mshikamano. na Wapalestina huku kukiwa na mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza.
Mawkib ni vituo vya huduma vilivyo katika maeneo ya kidini ya Waislamu wa madhehebu ya Shia au wakati wa matukio ya kidini ya Mashia ambapo wafanyaziara na watu wanaweza kupokea chakula, chai, na sharbat (vinywaji vitamu) na kupata sehemu ya kupumzika na malazi.