Toleo la tatu la Kongamano la Kimataifa la Nida al-Aqsa lililofungwa katika mji mtakatifu wa Iraq siku ya Jumanne.
Wasomi wa kidini na kisiasa na watu kutoka zaidi ya nchi 60 walihudhuria hafla hiyo ya siku mbili.
Wametoa taarifa mwishoni mwa mkutano huo ambapo wamesisitiza uungaji mkono wao wa dhati kwa wananchi wa Palestina na muqawama au mapambano ya silaha dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
Washiriki hao pia wametoa wito wa kukata kila aina ya uhusiano na utawala dhalimu wa Kizayuni.
Taarifa hiyo imepongeza zaidi misimamo ya serikali na watu wa Iraq katika mshikamano na taifa la Palestina.
Mkutano huo uliandaliwa na Kampeni ya Kimataifa ya Kurejea Wapalestina chini ya usimamizi wa Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS).
Washiriki walikutana na Sheikh Abdul Mahdi al-Karbalayi, Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) mwishoni mwa kongamano hilo.
Katika hotuba yake katika kikao hicho, Sheikh al-Karbalayi ameashiria umuhimu wa kuandaa hafla hiyo ya kila mwaka ili kupata uungaji mkono wa kimataifa kwa suala la Palestina, hasa kwa kuzingatia vita vya kikatili vinavyoendelea vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza.
3489503