IQNA

Arbaeen 1446

Sheikh Zakzaky aashiria uhusiano wa harakati ya Imam Hussein (AS) na uungaji mkono Palestina

17:34 - August 25, 2024
Habari ID: 3479327
IQNA- Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesisitiza kuwa misimamo yote ya uungaji mkono wa Palestina inatokana na harakati ya Imam Hussein (AS) na akasema: Kukusanyika kwetu leo ​​katika barabara ya kuelekea Karbala ni dhihirisho la ushindi harakati ya Imam Hussein (AS) na dalili zinaashiria kuangamizwa Israel na ushindi wa uhakika wa Gaza.

Kwa mujibu wa IQNA, Sheikh Ibrahim Zakzaky, ameyasema hayo katika Mawkib ya Wito wa Al-Aqsa katika mji wa Karbala alikoshiriki kumbukumbu ya Siku ya Arubaini ya Imam Hussein (AS) na kuongeza kuwa: Utawala ghasibu wa Israel umedhoofika na uko kwenye ncha ya kudidimia.

Sheikh Zakzaky amesema: Kuporomoka kwa utawala ghasibu kulianza kwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, na kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, utaangamia karibuni. Amesisitiza kuwa: "Hii sio kauli ya kutazamia ya kujipa matumaini, bali ushahidi uliopo unaonyesha hivyo."

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema: Leo na baada ya umwagaji damu mkubwa huko Gaza, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, Gaza itashinda, na baada ya hapo Palestina itashinda, na hivi karibuni tutatekeleza ibada ya Swala katika Msikiti wa Al-Aqswa. 

Vikiashiria mwenendo wa vita dhidi ya Ukanda wa Gaza na mauaji ya idadi kubwa ya wanajeshi wa Israel katika vita hivyo, vyombo vya habari vya utawala huo wa Kizayuni vimekiri kwamba, ahadi zilizotolewa na Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu, katika kipindi cha miezi 11 iliyopita kuhusu kushinda vita hivyo na kuiangamiza Hamas ni ndoto tupu na kauli za kuwahadaa watu. 

4233364

Kishikizo: ZAKZAKI arbaeen gaza
captcha