IQNA

Arbaeen 1446 H

Zaidi ya wafanyaziara milioni 21 wameshiriki matembezi Arbaeen 1446 H

23:52 - August 26, 2024
Habari ID: 3479332
IQNA - Zaidi ya wafanyaziara milioni 21 kutoka duniani kote walishiriki katika matembezi ya mwaka huu ya Arbaeen nchini Iraq, kwa mujibu wa Ofisi ya Haram Tukufu la Imam Hussein (AS), Karbala, Iraq.

Katika taarifa ya Jumapili, ofisi hiyo lilitangaza kwamba mazuwar au wafanyazaira 21,480,525 walikuwa wameshiriki katika tukio hilo kuu la kidini.

Arbaeen ni tukio la kidini linaloadhimishwa na Waislamu wa Shia katika siku ya arubaini baada ya Siku ya Ashura, ambayo ni kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na imamu wa tatu wa Shia katika mapambano ya Karbala mwaka 61 Hijria

Ni miongoni mwa safari kubwa zaidi za kila mwaka duniani, huku mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wakitembea kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arbaeen iliangukia tarehe 25 Agosti.

Kwa mujibu wa maafisa wa mpaka wa Iran, wafanyazaira wa Iran wapatao milioni 3.5 walikuwa wameingia Iraq kwa ajili ya Arbaeen kufikia Jumamosi.

Hakuna masuala ya ukosefu wa usalama yaliyoripotiwa katika matembezi ya mwaka huu, na hivyo Huduma ya Usalama wa Taifa ya Iraq imetangaza mafanikio ya mipango yake ya usalama.

3489647

Habari zinazohusiana
Kishikizo: arbaeen
captcha