"Tukio la kiibada na kiroho la matembezi ya Arbaeen limekuwa ishara kubwa ya umoja, mshikamano, na huruma kati ya mataifa na dini mbalimbali," alisema Jumatatu.
Kauli hiyo aliitoa katika ujumbe wake kwenye kongamano lililofanyika kuwaenzi watumishi wa safari na matembezi ya Arbaeen.
Ikumbukwe kuwa Arbaeen ni tukio la kidini linaloadhimishwa na Waislamu wa Shia katika siku ya arobaini baada ya Siku ya Ashura, kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na imamu wa tatu wa Shia.
Kila mwaka mamilioni watu hufunga safari na kuelekea Karbala, Iraq, mji lilipo kaburi la Imam Hussein (AS). Mjumuiko wa Arbaeen, ambao mwaka huu uliwaleta pamoja watu zaidi ya milioni 21, ni mjumuiko mubwa zaidi wa kidini duniani. miongoni mwa mahujaji kubwa zaidi za kila Aghalabu ya washiriki ni Waislamu wa madhehebu ya Shia, pamoja na Masunni wengi na wafuasi wa dini nyinginezo, ambao hutembea kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arbaeen iliangukia tarehe 25 Agosti.
Matembezi y Arbaeen "yana mandhari ya kuvutia na huadhimishwa katika kiwango cha kimataifa kila mwaka," aliongeza rais wa Iran.
"Tunaamini kwamba mafanikio ya kushiriki na kuhudumu katika njia hii adhimu haiwezekani bila ya neema ya Mwenyezi Mungu na moyo wa kweli wa kujitolea," alisema na kuongeza kuwa kila hatua inayochukuliwa katika nafasi yoyote ya kuhudumia idadi kubwa ya wafanyaziara na washiriki wa matembezi ya Arbaeen ya Imam Hussein (AS) huambatana thawabu za Mwenyezi Mungu.
“Nachukua fursa hii tena kutoa shukurani zangu na kwa watendaji wote, wasimamizi wa usalama, na wanahabari wote wanajitolea katka mjumuiko huu mkubwa wa kiroho, hasa juhudi za dhati za wasimamizi wa Mawkib (vituo ambavyo huto huduma za makkazi na malazi bila malipo kwa washiriki wa Arbaeen) wasomi wa kidini na wafadhili wa mikoa yetu ya mpakani, na pia ukarimu wa dhati wa taifa rafiki na serikali ya Iraq katika kuwahudumia mamilioni ya wafanyaziara,” aliongeza.
4241199