IQNA

Arbaeen 1446

Msimu wa Arbaeen ni fursa ya kukuza utamaduni wa kuhifadhi mazingira

22:41 - August 03, 2024
Habari ID: 3479221
IQNA - Matembezi ya kila mwaka ya Arbaeen ni fursa ya kueneza utamaduni wa kulinda mazingira.

Mohammad Hossein Bazgir, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Mazingira ya Mkoa wa Qom, ameyasema hayo alipohutubia mkutano wa wasimamizi wa Mawkib wa jimbo hilo utakaoanzishwa wakati wa msimu wa Arbaeen.

Mawkib ni vituo vya huduma vilivyo katika maeneo ya kidini ya Waislamu wa madhehebu ya Shia au wakati wa matukio ya kidini ya Mashia ambapo wafanyaziara na watu wanaweza kupokea chakula, chai, na sharbat (vinywaji vitamu). Kando ya njia ya matembezi ya Arbaeen, mawkib huanzishwa ili kutoa malazi, huduma za afya, masaji ya mwili na miguu, na ukarabati wa zana. Neno hili limekuwa likitumika sana katika utamaduni wa Mashia wa Iraq.

Bazgir amesisitiza umuhimu ambao Qur'ani Tukufu na Hadithizimeupa katika kulinda mazingira na akasema hilo pia limesisitizwa katika Katiba ya Iran.

Alitaja ushiriki wa wafanyaziyara zaidi ya milioni 20 katika matembezi ya Arbaeen na kusema ni tukio hilo ni munasaba katika kuendeleza utamaduni wa utunzaji wa mazingira.

Amesema wale wanaohudumu Mawkib wanapaswa kuwa mifano kwa katika suala la kuzingatia kanuni za ulinzi wa mazingira.

Wanaweza kufanya hivyo kwa kupunguza matumizi ya maji na nishati, kupunguza matumizi ya plastiki na kukusanya taka, alisema.

Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu  wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdii na jeshi la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.

Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi ya wasiokuwa Mashia humiminika Karbala, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) kufanya ibada za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala.

 

4229722

Habari zinazohusiana
Kishikizo: arbaeen mazingira
captcha