IQNA

Arbaeen 1446

Wafanyaziara kupata milo katika Haram ya Imam Ali (AS) hadi Mwisho wa Safar

23:39 - August 28, 2024
Habari ID: 3479341
IQNA – Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Ali (AS) huko Najaf, Iraq, imetangaza kuwahudumia wafanyaziara kwa kuwapa chakula katika eneo hilo takatifu hadi mwisho wa mwezi wa Hijri wa Safar.

Idadi kubwa ya wafanyaziara au Mazuwar wamekuwa wakitembelea kaburi hilo takatifu wakati wa msimu wa Arbaeen na kuna zaidi wanatarajiwa hadi mwisho wa Safar (Septemba 4).

Siku ya 28 ya Safar ni kumbukumbu ya kufariki kwa Mtume Muhammad (SAW) na kumbukumbu ya kifo cha kishahidi cha Imam Hassan Mujtaba (AS), na siku ya 30 ya mwezi (Septemba 4) ni kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Reza (AS).

Matukio haya ya maombolezo huvutia wafanyaziara  wengi kwenye eneo takatifu kutoka kote Iraq na nchi zingine.

Athir al-Tamimi idara hiyo, alisema kwamba kila siku hadi mwisho huo wa Safar, wafanyaziara hupata  zaidi ya milo 23,000, ikijumuisha 3,000 ya kiamsha kinywa, 12,000 chakula cha mchana, na 8,000 kwa chakula cha jioni.

Alisema zaidi ya watumishi 350 wa eneo hilo takatifu wanafanya kazi kila siku kutoa huduma hiyo.

Kulingana na al-Tamimi, mamilioni ya milo yalitolewa kwa wafanyaziara kwenye eneo hilo takatifu wakati wa Arbaeen.

Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Ali (AS) pia imekuwa ikiandaa programu mbalimbali za Qur'ani, kidini na kitamaduni kwa ajili ya wafanyaziara wa Arbaeen..

Arbaeen ni tukio la kidini linaloadhimishwa na Waislamu wa Shia katika siku ya arubaini baada ya Siku ya Ashura, ambayo ni kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na imamu wa tatu wa Shia katika mapambano ya Karbala mwaka 61 Hijria

Ni miongoni mwa safari kubwa zaidi za kila mwaka duniani, huku mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wakitembea kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arbaeen ilisadifiana na tarehe 25 Agosti.

Kwa mujibu wa maafisa wa mpaka wa Iran, wafanyazaira wa Iran wapatao milioni 3.5 walikuwa wameingia Iraq kwa ajili ya Arbaeen kufikia Jumamosi.

Hakuna masuala ya ukosefu wa usalama yaliyoripotiwa katika matembezi ya mwaka huu, na hivyo Huduma ya Usalama wa Taifa ya Iraq imetangaza mafanikio ya mipango yake ya usalama.

3489681

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: arbaeen
captcha