IQNA

Nigeria

Waislamu Mashia Nigeria wakosoa ghasia za Polisi dhidi ya waombolezaji wa Arbaeen

18:12 - September 02, 2024
Habari ID: 3479370
IQNA - Waislamu wa madhehebu ya Shia walifanya maandamano katika maeneo tofauti ya Nigeria kupinga ukatili wa hivi majuzi wa polisi dhidi ya wanawake na wasichana waliokuwa wanashiriki katika katika hafla za maombolezo ya Siku ya Arbaeen.

Walishutumu kuondolewa kwa nguvu kwa hijab kwa baadhi ya wasichana na wanawake walioshiriki katika matembezi ya Arbaeen wiki iliyopita.

Walielezea hatua hiyo kama ukiukaji mkubwa wa matukufu ya Kiislamu na haki za kibinafsi, kulingana na tovuti ya Akhbar Nigeria.

Waandamanaji hao pia walisema ni hatua ya aibu, uhalifu wa moja kwa moja, tusi kwa imani za kidini za watu wa nchi hiyo, na ukiukwaji wa uhuru wa kidini, katiba na sheria za kimataifa.

Maandamano hayo yalikuja baada ya kanda ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha maafisa wa polisi wakiwavua hijab wanawake kadhaa wa Kiislamu wakati wa hafla ya Arbaeen.

Waandamanaji hao walisema kuvaa hijabu ni sehemu ya dini na utamaduni wa Kiislamu na haki ya wanawake wa Kiislamu.

Walisema watawasilisha malalamiko katika Mahakama Kuu dhidi ya uvunjaji wa haki za wanawake wa Kiislamu.

Arbaeen ni tukio la kidini linaloadhimishwa na Waislamu hasa wa madhehebu ya Shia katika siku ya arobaini baada ya Siku ya Ashura, kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na Imam wa tatu wa Mashia.

4234543

Habari zinazohusiana
Kishikizo: nigeria arbaeen
captcha