IQNA

Arbaeen 1446

Zaidi ya Wairani 650,000 hadi sasa wameingai Iraq kwa ajili ya Arbaeen

20:35 - August 14, 2024
Habari ID: 3479279
IQNA - Makao Makuu makuu ya Iran ya Arbaeen yanasema idadi ya wafanyaziara wa Iran wanaosafiri kwenda Iraq kwa ajili ya kushiriki matembezi ya mwaka huu ya Arbaeen hadi sasa ni zaidi ya 650,000.

Katika taarifa yake siku ya Jumanne, makao makuu hayo yametangaza kuwa jumla ya wafanyaziara 659,540 kutoka Iran tayari wameingia Iraq kwa ajili ya matembezi hayo hayo ya kila mwaka.
Imeongeza kuwa karibu Wairani milioni 2.2 wamesajili majina yao katika mfumo wa Samah ili kushiriki katika ibada hiyo ya kilwa mwaka
Ikirejelea idadi kubwa ya maashiki wa Imam Hussein (AS) kutoka nchi tofauti wanaotarajiwa kushiriki katika safari hiyo ya kiroho, taarifa hiyo imewashauri wafanyaziara wa Iran kupunguza muda wao wa kukaa Iraq hususan katika mji mtakatifu wa Karbala.

Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu  wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdi na jeshi katili la la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.

Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi kubwa ya wasiokuwa Mashia humiminika  katika mji Karbala nchini Iraq, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) ili kushiriki katika shughuli za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala. Arbaeen ya mwaka huu inatarajiwa kuanguka mnamo Agosti 25, kulingana na kuonekana kwa mwezi.

Harakati ya mapambano ya Imam Hussein (AS) dhidi ya dhulma na ufisadi wa utawala wa Bani Umayya ilijaa hamasa, kujitolea na kusabilia kila kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, haki na uadilifu, na kwa sababu hiyo imegusa sana nyoyo za Waislamu na hata wapenda haki na kweli wasio Waislamu. Harakati hiyo ya Imam Hussein (AS) inaendelea kuibua vuguvugu na hamasa ya aina yake ndani ya nafsi za wapenzi wa mtukufu huyo.

/3489504

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: arbaeen
captcha