IQNA

Arbaeen 1446

Vidokezo kuhusu chakula kwa Mazuwar wa Arbaeen

15:36 - August 21, 2024
Habari ID: 3479308
IQNA - Huku mamilioni ya wafanyaziara au mazuwar wakiwa wanashiriki katika matembezi ya Arbaeen, wataalamu wanasisitiza umuhimu wa kudumisha mlo sahihi ili kuhakikisha afya na ustawi njiani.

Arbaeen ni tukio la kidini ambalo aghalabu huadhimishwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia katika siku ya arobaini baada ya Siku ya Ashura, kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na imamu wa tatu katika madhehebu ya  Shia. Matembezi ya Arbaeen ni miongoni mwa safari kubwa zaidi za kila mwaka duniani, huku mamilioni ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu wakitembea kwa kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani.

Pamoja na changamoto za kusafiri kwa muda mrefu, joto la juu, mazingira tofauti, kuzingatia chakula na vinywaji  ni muhimu. Pendekezo moja kuu ni kwa wafanyaziara kupanga mapema kwa kubeba vyakula ambavyo vina uwezekano mdogo wa kuharibika. Nyama, michuzi, na mayai huathirika zaidi na hali ya joto kali kama ilivyo hivi sasa Iraq na kuharibika haraka. Wafanyaziara wanashauriwa kuzingatia chakula ambacho kinabaki muda mrefu bila kuharibika.

Usafi sahihi unabaki kuwa msingi wa ulaji salama. Kuosha matunda na mboga mboga kabisa kabla ya kula ni jambo la lazima, kama vile kunawa mikono kwa sabuni na maji kabla ya milo.

Zaidi ya hayo, kula chakula ndani ya saa moja baada ya kutayarishwa kunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya ugonjwa unaosababishwa na chakula, jambo ambalo ni la kawaida wakati wa kusafiri.

Wataalamu wa lishe wanapendekeza kwamba wafanyaziara watumia vyakula vya kuchemshwa badala ya kuchomwa au kukaanga. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kukaanga au kuchoma kunaweza kupelekea chakula kutoiva ndani, na hivyo kuongeza hatari ya sumu ya chakula.

Kuwa na maji mwilini ni muhimu haswa mwaka huu ambapo matembezi ya Arbaeen yanaambatana na siku za joto za kiangazi. Maji yanatambulika kuwa kinywaji bora zaidi, ambapo inapendekezwa unywaji wa glasi 8 hadi 14 kwa siku ili mwili uwe na unyevu wa kutosha.

Vinywaji vya sukari na kafeini kama vile chai na kahawa havifai sana, kwani vinaweza kusababisha upungufu wa maji mwilini na huku vinyawji vitamu vikisababisha kuongezeka kiu. Kwa wale wanaopendelea aina mbalimbali, maji yaliyotiwa ladha na viungo kama vile maji ya minti au vipande vya matunda huwa mbadala bora.

Kwa lishe, dengu na sahani za maharagwe hupendekezwa sana. Vyakula hivi hutoa nishati endelevu na vinafaa zaidi kuliko vyakula vya haraka au milo nzito katika michuzi, ambayo inaweza kusaga wakati wa kusafiri.

Limau, iliyo na vitamini C nyingi, pia imeangaziwa kwa jukumu lake katika kuzuia kiharusi cha joto.

Inashauriwa kuwa mahujaji waepuke njaa ya muda mrefu, ambayo inaweza kusababisha uchovu na upungufu wa maji mwilini.

Vitafunio vyenye lishe kama vile matunda yaliyokaushwa, tende, matunda mapya, na karanga zenye chumvi kidogo hupendekezwa ili kudumisha viwango vya nishati. Hata hivyo, kiasi ni muhimu, kwani kula kupita kiasi kunaweza kuvuruga tumbo na hivyo kusababisha matatizo katika safari.

3489583

Habari zinazohusiana
Kishikizo: arbaeen
captcha