Jumuiya ya Waislamu Ulimwenguni (MWL) iliandaa hafla hiyo, ambayo ilihudhuriwa na mwanae marhum Sheikh Minshawi ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar Dakta Omar Muhammad Minshawi.
Katika hotuba yake, Omar alisema idadi kubwa ya wanafamilia yake ni wahifadhi na wasomaji wa Qur'ani.
Alibainisha kuwa baba yake alihifadhi Qur'ani yote akiwa na umri wa miaka 9 na kwamba alijifunza kusoma Qur'ani kutoka kwa baba yake na alishawishiwa na Sheikh Muhammad Rif'at, qari mwingine nguli wa Misri.
Ama kuhusu usomaji wake wa Qur'ani, Omar alisema Lahn na Sawt yake ni kama zile za baba yake.
Sheikh Muhammad Sidiq Minshawi aliyezaliwa Januari 20, 1920 katika mji wa Al Minshah katika Mkoa wa Sohag nchini Misri, alilelewa katika familia ya wasomaji wa Qur'ani.
Alijifunza Qur'ani nzima kwa moyo akiwa na umri wa miaka 9 na mwaka mmoja baadaye alianza kusoma Qur'ani.
Baada ya muda usio mrefu Minshawi akawa Qari mashuhuri katika mitindo ya Tahqiq na Tarteel.
Alisafiri katika nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Indonesia, Jordan, Saudi Arabia, Syria, Iraq, Pakistan na Sudan, kwa ajili ya kusoma Qur'ani.
Minshawi aliaga dunia na kurejea kwa Mola mnamo 1969 akiwa na umri wa miaka 49.
4235629