IQNA

Harakati za Qur'ani

Misri kuchukua hatua ya kisheria dhidi ya maqari ambao hawaheshimu Qur’ani Tukufu

21:56 - September 08, 2024
Habari ID: 3479400
IQNA - Jumuiya ya Wasomaji na Wahifadhi wa Qur'ani ya Misri iliwaonya maqari  dhidi ya kitendo chochote ambacho kinachukuliwa kuwa ni cha kutoheshimu Kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Katika taarifa, jumuiya hiyo ilisisitiza kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya qari yeyote, maarufu au asiyejulikana, ambaye anakidharau Kitabu Kitakatifu, tovuti ya Bawaba Ruz al-Yusuf iliripoti.

Mapema, Mkuu wa jumuiya hiyo Sheikh Mohamed Hashad alitoa wito kwa watu kuwaalika makari wenye uwezo katika programu zao za usomaji wa Qur'ani na kutafuta msaada kutoka kwa jumuiya katika suala hili.

Haya yanajiri baada ya qari aitwaye Samir Antaer kujibu simu yake ya mkono ya mobile  wakati akiwa anasoma Qur’ani.

Alikuwa akisoma Qur’ani Tuku katika ibada ya maombolezo wakati simu yake ya mkononi iliita. Aliacha kisomo na kujibu simu yake kabla ya kuendelea na kisomo.

Hatua yake hiyo imeibua shutuma nyingi nchini Misri. Hashad alionyesha kukerwa kwake sana na hatua hiyo na akamwita Antar ili amkanye kuhusu tabia yake hiyo.

Alisema alichofanya qari hakikufaa kutokana na hadhi tukufu ya Qur’ani.

 

4235253

Habari zinazohusiana
Kishikizo: misri qurani tukufu qari
captcha