IQNA

Nidhamu

Qari wa Misri Ahukumiwa Miezi 6 Jela

20:57 - March 08, 2024
Habari ID: 3478471
IQNA - Qari maarufu nchini Misri amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa tabia yake isiyo ya kawaida alipokuwa akisoma Qur’ani Tukufu hivi karibuni.

Sheikh Mohamed Ahmed Nasr Ali Qutb, anayejulikana kwa jina la Mohamed Nasr al-Taruti amepata kifungo cha jela.

Jumuiya ya Wasomaji na Wahifadhi wa Qur'ani nchini humo ilitangaza hayo, kwa mujibu wa Egypt Today.

Jumuiya hiyo ilisema itachukua msimamo thabiti dhidi ya ukiukaji unaofanywa wakati wa usomaji wa Qur’ani

Sheikh Mohamed Hashad, Mkuu wa Jumuiya hiyo amesema jumuiya inafanya juhudi za kulinda hadhi ya Kitabu Kitukufu katika jamii ya Misri na nafasi kuu ya nchi katika usomaji wa Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu.

Ndio maana chama kitachukua msimamo thabiti dhidi ya ukiukaji wowote katika uwanja huu, aliongeza.

Klipu ya mwenendo usiofaa wya Mohamed Nasr al-Taruti wakati wa kisomo cha hivi karibuni cha Qur'ani ni jambo ambalo limewakasirisha watu wengi nchini Misri.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100.

Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Qur'ani ni maarufu sana katika nchi ya Waarabu yenye Waislamu wengi na wengi wa maqari wakuu wa ulimwengu wa Kiislamu hapo awali na wa sasa wamekuwa Wamisri.

captcha