IQNA

Qiraa ya Qur'ani

Mahaba ya Qari Mutawalli Abdul Aal wa Misri katika Kusoma Qur'ani Tukufu

8:21 - April 28, 2024
Habari ID: 3478746
IQNA – Sheikh Mutawalli Abdul Aal Alikuwa qari mkubwa wa Misri ambaye alihifadhi shauku yake ya kusoma hadi siku za mwisho za uhai wake.

Ustadh Mutawalii Abdul Aal alizaliwa Aprili 1947 katika familia yenye kuzingatia dini nchini Misri na aliweza kuhifadhi Qur’ani akiwa na umri wa miaka 12. Baadaye alianza qiraa ya Qur’ani kwa kuiga mtindao ya usomaji wa Sheikh Abdulbasi na Sheikh Mustafa Ismail na hatimaye akaibua mtindo wake.

Alifanikiwa kutumbelea nchi mbali mbali duniani kama qarii na pia kama jaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani.

Ijumaa, Aprili 26, iliadhimisha siku yake ya kuzaliwa na tovuti ya habari ya Misri ya Youm7 ilizungumza na Najah al-Sayyid Ahmed, mke wa Abdul Aal na wanae kumhusu.
Najah al-Sayyid Ahmed alisema Abdul Aal alirithi sauti yake nzuri kutoka kwa baba yake.
Alisema alipokuwa akiisoma Qur'ani katika maisha yake yote, qari alidumisha Tawqa (kumcha Mungu).
Alikuwa mtu anayeaminika na mwenye roho iliyotakaswa na mlango wa nyumba yake ulikuwa wazi kwa watu wote, alisema.
Pia alisema kwamba watu wengi, ikiwa ni pamoja na Asia Mashariki, walisilimu baada ya kusikiliza kisomo chake cha Qur'ani
Binti wa Abdul Aal, Nadia, ambaye ni mhifadhi wa Qur'an na mwalimu wa lugha ya Kiingereza, alisema baba yake alijifunza Qur'ani katika Maktab (shule ya zamani ya Qur'ani).
Anasema  Sheikha Maryam aliyekuwa na ulemavu wa macho alimfundisha Quran na alikuwa akimzungumzia kama mwalimu wake wa kwanza.
Salah, mtoto wa qari mashuhuri, aliiambia Youm7 kwamba baba yake alipata umaarufu baada ya kurekodi usomaji wake wa Surah Yusuf na baadhi ya Sura zingine za Quran mnamo 1984.
Baada ya hapo, alibainisha, baba yake alipata mafuriko ya mialiko ya kusafiri katika nchi mbalimbali kusoma Quran.
Salah pia alibainisha kwamba baba yake alidumisha shauku yake ya usomaji wa Kitabu Kitakatifu hadi dakika za mwisho za maisha yake.
Pia alisema kwamba makari mashuhuri kama Mohamed Abdul Whab Tantawi, Farajullah Shazli, Abdul Fattah Taruti, na Ismail Tantawi walisoma Kurani kwenye mazishi ya baba yake.
Hapa chini ni kanda ya video ya usomaji wa Qur'ani wa  Sheikh Mutawalli Abdul Aal:

 

 

 

 

 

3488095

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qari misri qurani tukufu
captcha