Haya ni kwa mujibu wa Hujjatul Islam Seyed Mostafa Hosseini Neyshabouri, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Tabligh (uenezi) ya ICRO.
Aliandika katika makala kwa IQNA kwamba itasonga mbele katika njia ya kuhuisha Ummah ulioungana wa Kiislamu chini ya mhimili wa pamoja wa mafundisho ya Qur'ani. Zifuatazo ni nukuu kutoka kwa kifungu hicho:
Kongamano la 20 la Kimataifa la Kiislamu liliandaliwa mjini Moscow, Urusi (Russia), na Jukwaa la Kimataifa la Kiislamu, Mamlaka ya Kiroho ya Waislamu wa Shirikisho la Urusi, na Baraza la Mufti la Urusi chini ya mada: "Njia ya Amani: Mazungumzo kama Msingi wa Kuishi kwa Maelewano." .”
Wanazuoni wa Kiislamu, wanafikra na Mamufti kutoka nchi 48 walishiriki katika kongamano hilo mnamo Septemba 20-21.
Katika hafla hiyo, Mkuu wa ICRO Hujjatul Mohammad Mehdi Imanipour, ambaye aliwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alipendekeza kuanzishwa kwa bunge la Qur'ani la ulimwengu wa Kiislamu.
Malengo ambayo bunge kama hilo linaweza kufuata ni pamoja na kutambulisha na kutangaza mafundisho ya Qur'ani na kwamba Qur'ani ni ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa walimwengu, kuzuia kuenea kwa dhana potofu kuhusu Qur'ani, kuunganisha shughuli za Qur'ani na kuendeleza vituo vya Dar-ul-Quran duniani. Aidha bunge hilo litabanisha kivitendo mafundisho ya Qur'ani katika ngazi ya kimataifa, kusaidia wanaharakati wa Qur'ani hasa maqari, wahifadhi, wafasiri, watafiti, wasanii na wengine wanaofanya kazi katika ngazi ya kimataifa, kuinua kiwango cha ushirikiano wa kimataifa na mada ya Qur'ani, na mipango ya kimkakati ya kufufua utamaduni na mtindo wa maisha wa Qur'ani.
3490024