IQNA

Diplomasia ya Qur'ani

Mkutano wa Risalatallah unalenga kukuza mafundisho ya Qur'ani ulimwenguni

18:41 - October 14, 2024
Habari ID: 3479592
IQNA - Kongamano lijalo la Risalatallah linalenga kueneza mafundisho ya Qur'ani Tukufu duniani, amesema mwanazuoni mwandamizi wa Kiislamu.

Hujjatul Islam Seyed Mostafa Hosseini Neyshaburi, Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Qur'ani na Uenezi cha Shirika la Iran la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu (ICRO) aliyasema hayo jana Jumapili katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran.

Amesema kuhuisha udiplomasia wa Qur'ani miongoni mwa asasi na shakhsia wa ulimwengu wa Kiislamu na kubainisha ipasavyo mafundisho ya Qur'ani kwa walimwengu pia ni miongoni mwa malengo ya mkutano huo.

Lengo lingine linalofuatiliwa ni kutoa mafunzo kwa wanaharakati wa Qur'ani na kwa ajili hiyo, vituo vya Dar-ul-Quran vimeanzishwa katika nchi kama Bosnia na Herzegovina, alisema.

"Moja ya malengo yetu mengine ni (kutayarisha uwanja wa kutambulisha) na kueleza mawazo ya kisasa ya Qur'ani na kazi bora zaidi zilizoandikwa katika nyanja za sayansi, mafundisho na sanaa za Qur'ani."

Amebainisha kuwa, toleo la kwanza la kongamano hilo la kimataifa lililoandaliwa mapema mwaka huu lilikaribishwa sana na nchi za Kiislamu.

Ilisaidia nchi zinazoshiriki kujifunza zaidi kuhusu uwezo wa Kurani wa kila mmoja wao, Hujjatl Islam Hosseini Neyshaburi alisema.

"Tunajaribu kubadilisha maelewano yaliyofikiwa katika mkutano huu kuwa mipango ya kiutendaji."

Alisema mada kuu ya kongamano la mwaka huu itakuwa mtindo wa maisha wa Kiislamu-Qur'ani.

Risalatallah Conference Aims to Promote Quranic Teachings Globally  

Malaysia na Indonesia ndizo zitaandaa mkutano huo, kwa mujibu wa afisa huyo. Kongamano hilo litafanyika Alhamisi, Oktoba 17, Kuala Lumpur na kisha Alhamisi inayofuata, Oktoba 24, huko Jakarta, alisema.

Wanazuoni, wanafikra na wawakilishi wa vituo vya Qur'ani kutoka Iran, Tunisia, Misri, Iraq, Russia, Lebanon, Malaysia, Senegal, Thailand, India na Pakistan waliwasilisha maoni yao kuhusu toleo la kwanza la kongamano hilo mjini Tehran mnamo Januari 2024.

 242061

captcha