IQNA

Warsha ya kujadili 'Qiraa na Tajwid' ya Qur'ani barani Afrika

18:00 - November 25, 2021
Habari ID: 3474600
TEHRAN (IQNA)- Warsh ya kujadili 'Hali ya Qiraa na Tajwid ya Qur'ani Tukufu Barani Afrika' imepangwa kufanyika wiki ijayo kwa njia ya intaneti.

Kwa mujibu wa taarifa, warsha hiyo itakayoanyika Jumatatu Novemba 29 imeandaliwa na Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu Iran (ICRO) limepanga warsha hiyo kwa ushirkiano na  Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) pamoja na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Algeria.

Wataalamu wa Qur'ani Tukufu kutoka Iran na Algeria watahutubu katika kikao hicho. Imedokezwa kuwa kati ya wazungumzaji wa warsha hiyo ni msomi wa Qur'ani kutoka Algeria Sheikh Nureddin Abu Lahya, Mkuu wa  Jumuiya ya Maulamaa na Wahubiri wa Sahara Sheikh Yusuf Mushriya na Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Algeria Sayyid Jalal Miraghaei pamoja na mtaalamu wa masuala ya Qur'ani ICRO Sayyid Hassam Esmati ambaye aliwahi kuwa Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Senegal.

Kikao hicho kitafanyika kwa lugha ya Kiarabu kuanzia saa nane na nusu saa za Afrika Mashariki na kuendelea kwa saa nzima. Wanaotaka kufuatilia kikao hicho kwa njia ya skype wanaweza kubonyeza hapa.

4016085

captcha