IQNA

Umoja wa Kiislamu

Ustaarabu Mpya wa Kiislamu Unawezekana tu kupitia umoja wa Waislamu

18:55 - May 27, 2022
Habari ID: 3475302
TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Shirika la Iran la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu (ICRO) amesema ustaarabu mpya wa Kiislamu unaweza kupatikana tu kupitia umoja wa Waislamu.

Akizungumza katika mkutano na wanazuoni wa Kisunni wa Nepal ambao wako safarini nchini Iran, Hujjatul Islam Mohammad Mehdi Imanipour alisisitiza haja ya ukuruba kati ya madhehebu za Kiislamu, na kusema bila kuwepo ukuruba kama huo, basi hakutakuwa na ustaarabu mpya wa Kiislamu.

Alisisitiza kwamba Waislamu wote ni ndugu, na kuongeza kuwa mazungumzo ya kielimu ni utangulizi wa kuundwa kwa Ummah Wahidah (umma Kiislamu ulioungana).

Hujjatul Islam Imanipour ameashiria njama ya vyombo vya habari vya Magharibi ya kuchafua sura ya Uislamu duniani na kusema iwapo Waislamu wataendelea kushikamana na mafundisho ya dini hiyo, madola ya kibebebru duniani hayawezi kuwadhuru.

Kwingineko katika matamshi yake, mwanazuoni huyo wa Kiislamu ameashiria shughuli za ICRO na kubainisha kwamba ICRO ina jukumu la kutekeleza shughuli za kitamaduni za Iran katika nchi nyingine na kuendeleza fikra na mafundisho ya Kiislamu duniani ili kuhuisha ustaarabu wa Kiislamu.

Kukuza utamaduni wa Qur'ani, kufundisha mitazamo ya Qur'ani na tafsiri ya Qur'ani, kutafakari kuhusu aya Qur'ani, kukurubisha madhehebu za Kiislamu, kustawisha mazungumzo ya kidini na kitamaduni, na ushirikiano wa vyuo vikuu ni miongoni mwa shughuli za ICRO nje ya nchi, alisema.

Baadhi ya wajumbe wa ujumbe wa Nepal na pia wamesisitiza umuhimu wa umoja katika ulimwengu wa Kiislamu.

Aidha  wamepongeza mapenzi ya Uislamu waliyonayo  watu wa Iran na kutoa wito wa kuendeleza ushirikiano na Iran.

4059690

captcha