IQNA

Jinai za Israel

Wapalestina wapongeza UN kwa kuorodhesha Israel kama 'muuaji watoto'

21:45 - June 08, 2024
Habari ID: 3478950
IQNA - Maafisa wa Palestina na makundi ya muqawama wamekaribisha uamuzi wa Umoja wa Mataifa wa kuuongeza utawala wa Israel kwenye 'Orodha ya Aibu' kwa kuua watoto katika vita vya Gaza.

Umoja wa Mataifa umeongeza jeshi la Israel kwenye "orodha ya aibu" ya kila mwaka ya wahalifu wanaoua watoto.

Gilad Erdan, balozi wa utawala wa Israel katika Umoja wa Mataifa, alifahamishwa rasmi kuhusu uamuzi huo ambao umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, siku ya Ijumaa.

Orodha hiyo imeambatanishwa na ripoti kuhusu watoto na mizozo ya kivita ambayo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa huwasilisha kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kila mwaka.

Ripoti hiyo inahusu ukatili kama vile kuua na kulemaza watoto, kuwafanyia unyanyasaji wa kijinsia, kuwateka nyara au kuwasajili watoto kwenye vita, kuzia misaada ya watoto, na kulenga shule na hospitali.

Orodha hiyo imetangazwa wakati utawala haramu wa Israel unaendeleza vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7 mwaka jana.

Mashambulizi hayo ya kijeshi ya Israel hadi sasa yamesababisha vifo vya Wapalestina 36,731 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Siku ya Ijumaa, serikali ya Palestina katika Ukanda  Gaza iliripoti kuwa, tangu kuanza mashambulizi hayo, jeshi la Israel limeua zaidi ya watoto 15,517.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa zaidi ya watoto 17,000 wa Gaza hadi sasa pia wamepoteza mzazi mmoja au wote wawili.

Takriban watoto 3,500 wa Gaza wamekuwa wakipambana na utapiamlo ambao umesababishwa na vita hivyo.

Ikijibu uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa, Mamlaka ya Palestina (PA) imeutaja kuwa ni hatua sahihi ya kuadhibu utawala wa Tel Aviv.

Naye Izzat al-Risheq, mjumbe mkuu wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, pia alikaribisha hatua hiyo ya Umoja wa Mataifa.

Amesema kuingizwa kwa utawala wa Israel katika "Orodha ya Aibu" kwa mauaji yake ya watoto wa Kipalestina kumewakasirisha sana  wanajeshi wa utawala huo, waziri mkuu na maafisa wengine.

Alibainisha kuwa Israel sasa imetengwa na kufunguliwa mashitaka katika mahakama za kimataifa.

Hapo awali Hamas iliutaka Umoja wa Mataifa kuuorodhesha Israel katika orodha ya aibu ya wanaouawa kutokana na utawala huo katili kuendelea kuwaua watoto wasio na hatia wa Kipalestina.

3488659

captcha