IQNA

Harakati za Qur'ani

Mwanazuoni wa Kiislamu abainisha Sifa muhimu za Maqari wa Qur’ani

22:51 - December 04, 2024
Habari ID: 3479852
IQNA – Hafidh wa Qur'ani ambaye pia ni mwanazuoni wa Kiislamu ametaja sifa nyingi ambazo anaamini ni muhimu kwa qari kuwa nazo kwa ajili ya usomaji wenye taathira.

Hujjatul Islam Haj-Abolghasem Doolabi, hafidh mashuhuri wa Qur'ani nchini Iran ambaye pia na mjumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu, aliyasema hayo alipokuwa akihutubia katika Kikao cha 19 cha Wanazuoni Mashuhuri wa Qur'ani, Maqari na Wahifadhi wa Qur'ani kilichofanyika na Baraza Kuu la Qur'ani mjini. Tehran wiki iliyopita.

Amesisitiza jukumu muhimu la wasomaji wa Qur'ani katika kuwasilisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu, akionyesha sifa kuu zinazofanya usomaji wao kuwa na athari. Akizungumza katika hafla ya hivi karibuni, alisema:

"Kwa kuzingatia aya ya 39 ya Surah Al-Ahzab, aya zenye kung'aa za Qur'ani ni zana bora zaidi za mawasiliano. Qari lazima watimize kazi yao kwa kuzingatia lengo la Mwenyezi Mungu la kueneza Qur’ani kupitia sauti ya kupendeza."

Akitoa mfano wa Mus‘ab ibn Umair, shakhsia mashuhuri wa Kiislamu, Haj-Abolghasem alibainisha kwamba alijumuisha ubora wa mhubiri na qari. "Wakati watu wa jamii ya Ansar walipomwomba Mtume (SAW) awatumIe mtu wa kuwafundisha, aliona hakuna mtu mwingine anayefaa zaidi kuliko Mus'ab, ambaye alitumia usomaji wa Qur’ani kama chombo chenye nguvu cha da'wah," alieleza.

Msomi huyo amesisitiza umuhimu wa kutambua ukuu wa Qur'ani, akisisitiza kwamba ufahamu huu lazima utangulie ujuzi mwingine kama vile ubora wa sauti. "Quran ni baraka kubwa, ambayo inahakikisha ustawi na uongozi wa umma wa Kiislamu," alisema, akibainisha kwamba qari lazima aingize ukweli huu ndani kabla ya kujaribu kuushiriki.

Msomi huyo amesisitiza uaminifu kama sifa ya msingi kwa qari, akisema, "Lazima maqari wajitolee kwenye njia hii takatifu bila kutafuta faida ya kifedha, sawa na Mitume (SAW) ambao hawakuwahi kudai malipo kwa ajili ya kueneza imani. Hata hivyo, msaada wa vitendo kutoka kwa fedha za umma ni muhimu kukidhi mahitaji yao ya kimsingi."

Pia alikazia umuhimu wa uchaji Mungu, unyenyekevu, na kiasi. "Qari lazima awe kielellzo cha mafundisho ya Qur’ani na kuepuka majivuno yanayotokana na umaarufu wao," aliongeza.

Aidha ametoa wito kwa maqari kudumisha mavazi yanayofaa kwa jukumu lao. "Kulikuwa na mpango wa kubuni mavazi rasmi kwa wasomaji wa Qur'ani kwenye hafla za umma, lakini bado haujatimia," alisema, akizitaka mamlaka kurejea mpango huo.

Mwanachuoni huyo amesisitiza zaidi umuhimu wa kuhifadhi Qur’ani. Akizungumzia mafundisho ya marehemu Sheikh Shahat Muhammad Anwar, alisema: "Qari mwenye ufanisi lazima pia awe hafidh. Hii inawawezesha kuzingatia kufikisha maana za Qur’ani badala ya kushughulishwa na matamshi tu."

3490934

Kishikizo: qurani tukufu qari iran
captcha