IQNA

Msikiti wa Cairo waandaa hafla ya Khatmul Quran kwa Wanawake

17:13 - January 29, 2024
Habari ID: 3478270
IQNA – Kiikao cha Khatmul Quran (kusoma Qur'ani Tukufu kutoka mwanzo hadi mwisho) kimefanyika kwa wanawake katika msikiti katika mji mkuu wa Misri.

Kikao hicho kimeandaliwa katika Msikiti wa Al-Sayyida Nafisa baada ya sala ya adhuhuri Jumatatu, Waziri wa Awqaf wa Misri Sheikh Mohammed Mukhtar Gomma amesem.

Aliongeza kuwa wizara hiyo pia inapanga kuandaa kongamano 11 katika vituo vya Kiislamu wiki ijayo ili kujadili masuala kadhaa makubwa ya kidini na kitamaduni.

Mipango hii inafanyika kama sehemu ya jukumu la wizara katika kukuza maoni ya wastani, kuongeza uelewa kuhusu masuala ya kitamaduni na kijamii, na kueneza maadili katika jamii, alisema.

Pia zinalenga kukuza ufahamu wa kidini na kupambana na itikadi kali, aliongeza.

Katika miaka ya hivi karibuni, Wizara ya Wakfu ya Misri imeweka msisitizo mkubwa katika kukuza mawazo ambayo inayaona kuwa ya wastani.

Baadhi ya wakosoaji wanasema msisitizo wa kile kinachoitwa "mtazamo wa wastani" unaendana na sera mpya za serikali ya Misri zinazolenga kuweka vikwazo kwa shughuli za taasisi za kidini.

Wanasema ukosoaji wowote wa sera za serikali au pingamizi dhidi ya ufisadi hutajwa kama maoni ya itikadi kali na hivyo kuchukuliwa hatua.

3486993

captcha