IQNA

Idhaa  ya Qur’ani ya Misri kusitisha matangazo ya biashara

23:19 - December 30, 2024
Habari ID: 3479976
IQNA – Matangazo ya biashara hayatatangazwa tena kwenye kituo cha Idhaa au Radio ya Qur'ani ya Misri kuanzia Januari 1, 2025.

Hii inakuja baada ya Mamlaka ya Kitaifa ya Habari (NMA) kuamua Jumapili kupiga marufuku matangazo ya biashara kwenye Idhaa ya Qur’ani kufuatia malalamiko kutoka kwa umma na viongozi wa taasisi rasmi za kidini.

Uamuzi huu unafuata marufuku ya NMA, iliyofanywa karibu wiki moja mapema, ya kuwaalika wachawi na wanaastrologia kwenye vituo vyote vyaa televisheni, vituo vya radio, na majukwaa ya kidijitali.

NMA, inayoongozwa na Ahmed El-Moslemany, iliidhinisha pendekezo kutoka kwa Kamati ya Salamu na Sera za Matangazo.

Kwa hivyo, matangazo ya biashara hayatatangazwa tena kwenye Radio ya Qur’an kuanzia mwaka mpya.

Radio ya Quran ya Misri ilianzishwa mwaka 1964,  nina zaidi ya wasikilizaji milioni 60 nchini Misri na ulimwengu wa Kiislamu.

Pia, El-Moslemany alimshukuru Khaled Abdel Aziz, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Vyombo vya Habari, kwa juhudi zake na Wizara ya Fedha kwa kufidia upotevu wowote unaowezekana wa mapato ya matangazo kufuatia kusitishwa matangazo ya biashara katika  Radio ya Quran ya Misri kwenda vituo vingine.

3491259

Kishikizo: misri idhaa ya qurani
captcha