IQNA

Muqawama

Mufti Mkuu wa Oman: Njia ya Shahidi Haniya itaendelea

14:52 - August 02, 2024
Habari ID: 3479217
IQNA - Mufti Mkuu wa Oman amelaani mauaji ya utawala wa Israel dhidi ya Ismail Haniya, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Hamas.

Katika chapisho kupitia akaunti yake ya X, Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili alisema kifo cha Haniyah katika shambulio la kinyama la utawala wa Israel kilikuwa cha kusikitisha na cha kusikitisha.

Alisisitiza, hata hivyo, kwamba muqawama au mapamabno ya Palestina yataendelea kuwa hai na njia ya Shahidi Haniya itaendelea.

Muqawama bado uko hai na utaendelea na mapambano yake katika njia ya kuikomboa ardhi takatifu ya Palestina, aliongeza.

Mauaji hayo yataongeza tu nguvu, uimara na azma ya muqawama, kama Shahidi Haniyeh angesema, Sheikh Al Khalili alisema.

Mufti huyo mkuu wa Oman alitoa salamu za rambirambi kwa Umma wa Kiislamu, wananchi wa Palestina na harakati za muqawama katika eneo hilo kutokana na kuuawa shahidi Haniya.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilitangaza Jumatano asubuhi kwamba Haniya na mmoja wa walinzi wake waliuawa katika makazi yao jijini Tehran.

Taarifa hiyo ilionyesha kuwa shambulio hilo linachunguzwa, na matokeo yanatarajiwa kutangazwa baadaye.Haniya alikuwa Tehran kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Iran Masoud Pezeshkian.

 4229533

Habari zinazohusiana
captcha