IQNA

Muqawama

Hamas yathibitisha kuafiki mapatano ya usitishaji vita Gaza

23:38 - January 15, 2025
Habari ID: 3480060
IQNA- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina (Hamas) imeidhinisha pendekezo la kusimamisha mapigano kwa Ukanda wa Gaza ambayo yamefikiwa kwa upatanishi wa Misri na Qatar.

Wapatanishi nchini Qatar wamekuwa wakifanya juhudi za kupata makubaliano kati ya Israel na Hamas ili kumaliza zaidi ya miezi 15 ya vita vya kimbari vinavyoendelezwa na utawala haramu wa Israel huko Gaza. Kwa mujibu wa mapatano hayo, Hamas itawaachilia mateka wa Israel kwa kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina.

Maelezo kuhusu masharti na awamu za makubaliano hayo bado hayajatangazwa, lakini Hamas imesema katika taarifa kwamba ujumbe wake, unaoongozwa na Khalil al-Hayya, mwanachama wa Baraza la Kutunga Sheria la kundi hilo, umekabidhi idhini yake kwa maandishi kwa wapatanishi nchini Qatar na Misri.

"Uongozi wa Hamas umewasilisha muda mfupi uliopita kwa ndugu wapatanishi majibu yake kwa pendekezo la makubaliano ya kusimamisha mapigano," harakati hiyo imesema katika taarifa yake. "Ofisi ya kisiasa ya kundi hilo ilifanya mkutano wa dharura kujadili pendekezo lililowasilishwa na wapatanishi."

"Harakati imechukua hatua kwa uwajibikaji na mtazamo mzuri, kwa kuzingatia uwajibikaji wake kwa watu wetu wa subira na istikama katika Ukanda wa Gaza, kwa kusimamisha ukatili wa Kizayuni dhidi yao, na kukomesha mauaji na vita vya kimbari wanavyokabiliwa navyo," imesema.

Barabara za Gaza zimegubikwa kwa furaha baada ya habari za kusimamishwa kwa mapigano kuanza kusikika. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, watu waliohamishwa wataruhusiwa kurudi kwa miguu kuanzia siku ya saba ya kusimamishwa kwa mapigano, bila upekuzi wowote. Hata hivyo, magari yanayorudi kutoka Gaza kusini kwenda kaskazini yatafanyiwa ukaguzi kwa kutumia vifaa vya X-ray vinavyofanya kazi kwa ushirikiano wa kampuni za Misri na Qatar.

Vikosi vya nchi kavu vya utawala wa Israel vitaondoka taratibu kutoka kwenye korido za Netzarim na Philadelphi. Jeshi hilo la Israel litaondoka ndani ya mita 700 ndani ya Gaza. Kuondoka kwa Netzarim kutakuwa kwa haraka. Kuondoka kwa korido ya Philadelphi kutaaanza taratibu baada ya siku 40 hadi 50 kutoka kuanza kwa awamu ya kwanza.

Utawala wa Israel pia utaacha kudhibiti Korido Philadelphi, kando ya mpaka wa Gaza na Misri. Israel itafungua mpaka wa Rafah na Misri baada ya siku saba za kuanza kwa awamu ya kwanza.

Harakati za muqawama Palestina zitaachilia wafungwa 33 kwa kubadilishana na mateka 2,000 kutoka Gaza. Israel itaruhusu watu waliojeruhiwa Gaza kusafiri kupokea matibabu.

Kuna upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya wanachama wa baraza la mawaziri la Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ambao hawatai kusimamishwa kwa mapigano Gaza. Hata hivyo, vyombo vya habari vya Israel vilidokeza kuna uungwaji mkono wa kutosha katika Knesset na baraza la vita kwa makubaliano hayo.

Kura kuhusu maptano hayo inatarajiwa kufanyika Alhamisi katika utawala wa Israel. Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli Gideon Saar alisema anakata ziara yake Ulaya kwa kifupi ili kushiriki katika kura hiyo za makubaliano ya Gaza.

Waziri wa mrengo wa kulia wa Israeli Itamar Ben-Gvir ametoa wito kwa waziri wa fedha Bezalel Smotrich kujiuzulu pamoja naye kama makubaliano ya kusimamisha mapigano yatatekelezwa, kwa mujibu wa taarifa yake kwenye Telegram. "Makubaliano yanayoibuka ni makubaliano ya kujisalimisha kwa Hamas... Kwa hiyo, namwomba rafiki yangu Bezalel Smotrich ajiunge nami na kushirikiana katika kupinga makubaliano hayo," Ben-Gvir alisema.

"Hatutakuwa sehemu ya makubaliano ya kujisalimisha ambayo yatashirikisha kuachiliwa kwa wafungwa wengi wa Kipalestina."

Israeli imeshindwa kufikia malengo yoyote iliyoyatangaza ya vita, licha ya kuua zaidi ya Wapalestina 46,700, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kubomoa karibu eneo lote la pwani.

Israeli ilianzisha vita vya kimbari Gaza mnamo Oktoba 7, 2023, kufuatia shambulio la kushtukiza la makundi ya muqawama wa Kipalestina. Lengo la vita lilikuwa kuangamiza Hamas na kurudisha mateka. Hatahivyo Israel haijawez kuangamiza Hamas na imeshindwa kukomboa Waisraeli wanaoshikiliwa kma wafungwa wa kivita na Hamas.

4260161

Habari zinazohusiana
captcha