IQNA

Muqawama

Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran: Utawala wa Kizayuni umelazimik kusitisha vita baada ya kukata tamaa

22:37 - January 18, 2025
Habari ID: 3480073
IQNA – Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema kuwa utawala wa Kizayuni umelazimika kusitisha mapigano na Harakati ya Kiislamu ya Ukombozi wa Palestina, Hamas, huko kwa sababu ya udhaifu na kukata tamaa. Hii ni moja ya heshima za mstari wa mbele wa upinzani, alisema Hujjatul-Islam Gholam Hossein Mohseni Ejei, akihutubia mkutano wa 13 wa "Gaza; Alama ya Muqawama" jijini Tehran.

Amewaenzi mashahidi wa muqawam, hasa wale wa Gaza, Palestina, Lebanon na Yemen. Ahadi za Mwenyezi Mungu sasa ni wazi zaidi na zinaeleweka zaidi, na aya za Mwenyezi Mungu  zimepata maana dhahiri zaidi kwa viwango vyote vya ubinadamu leo, alisema.

"Tulishuhudia jinsi wale wanaojitahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, walisimama imara na kukabiliana na changamoto njiani, walivyoshinda na kuheshimiwa," alisema. Akibainisha kuwa utawala wa Kizayuni umekuwa ukifanya uhalifu kwa msaada wa Marekani, Uingereza na serikali nyingine za Magharibi kwa zaidi ya miaka 75, alisema taifa la Palestina limekabiliana utawala huo na wafuasi wake wote kwa zaidi ya miongo saba.

Leo, ahadi ya Mwenyezi imetimizwa na watu wema wa dunia wana majukumu mawili, alisema Hujjatul-Islam Mohseni Ejei. "Jukumu moja ni kufichua uhalifu unaofanywa na utawala wa Israeli na wafuasi wake na jingine ni kuunga mkono taifa lililodhulumiwa na lenye nguvu (la Palestina)."

Aliisifu makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yanamaliza vita katika Ukanda wa Gaza na kusema kuwa utawala wa Kizayuni haukufikia malengo yake yoyote katika vita hivi vya mauaji ya kimbari. "Utawala wa Kizayuni uko katika hali ya kukata tamaa kabisa leo na umekubali kusitisha mapigano kwa sababu ya kukata tamaa na udhaifu," alisisitiza.

"Lazima tuendelee katika njia ya (wapiganaji wa Muqawama), na ikiwa tutavumilia katika njia hii kwa subira, mapambano, umoja, na mshikamano, tutafanikiwa bila shaka."

Qatar ilitangaza Jumatano kwamba Israel na kundi la muqawama la Hamas la Palestina walikubaliana kusitisha mapigano.

349149

Kishikizo: mapatano gaza hamas israel
captcha