Hujjatul Hamid Reza Arbab Soleimani, mkurugenzi wa maonyesho na ambaye pia ni Naibu Waziri Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu ya Iran anayeshughulikia masuala ya Qur’ani na Etrat amezungumza na IQNA pembeni mwa tukio hilo siku ya Ijumaa.
"Maonyesho haya yana tofauti kubwa," alisema Arbab Soleimani. "Inajumuisha sehemu za watoto, tafiti na mijadala ya kisayansi, matumizi ya akili mnemba, na maonyesho ya kisanii, na kuyafanya kuwa na mvuto mkubwa."
Akitumia mfano wa wito Adhana, alisisitiza kuwa maonyesho hayo yanapaswa kuhamasisha hatua.
"Kama vile tunavyoamka kwa ibada tunaposikia adhana ya Alfajiri, maonyesho haya yanapaswa kusababisha mwitikio kama huo - kuhamasisha mawazo mapya, kubadilishana uzoefu, na kukuza utamaduni wa ushirikiano wa Qur’ani," alisema.
Alibainisha kuwa ushiriki mzuri wa watoto na watu wazima unaonyesha shauku kubwa ya jamii katika shughuli za Qur’ani. "Shauku hii inaonyesha kwamba watu wana hamu ya mipango ya Qur’ani. Kadri tunavyowapa njia mpya na za ubunifu, ndivyo uhusiano wao na Qur’ani utakavyokua," alisema.
"Awali ni ushirika na Qur’ani, kisha tafakuri, na hatimaye, hatua kulingana na mafundisho yake," aliongeza.
Maonyesho hayo yalifunguliwa siku ya Jumatano na yataendelea hadi Machi 16. Maonyesho ya mwaka huu yanajumuisha vipindi mbalimbali, ikiwemo vikao maalum, warsha za elimu, mikusanyiko ya Qur’ani, na shughuli maalum kwa watoto na vijana.
Toleo la 32 linachukua takriban mita za mraba 20,000, likihusisha sehemu 37 .
Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na huandaliwa Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu ya Iran.