Aliyasema haya alipohutubia Kongamano la 30 la Kuwaenzi Wahudumu wa Qur'ani huko Tehran. Hafla hiyo ilifanyika Jumapili pembeni mwa usiku wa mwisho wa Maonyesho ya 32 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran katika Ukumbi wa Mosalla Imam Khomeini.
“Moja ya changamoto ninazoziona katika jamii leo ni ukosefu wa utekelezaji linapokuja suala la mafundisho ya Qur'ani Tukufu,” alisema Dakta Pezeshkian.
Akinukuu aya ya 9 ya Surah Al-Isra' inayosema, “Hakika hii Qur´ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa,” amesisitiza kuwa mafundisho haya yanapaswa kudhihirika katika nyanja zote za maisha.
“Hatuwezi kudai kwamba Qur'ani inatuonyesha njia huku, wakati huo huo, tuna mapungufu katika tabia, maarifa, maadili, na usimamizi,” aliongeza.
Rais amesisitiza umuhimu wa kuwalea wanafunzi na vijana wawe wanachama wa jamii wenye athari. “Tunaisoma Qur'ani kwa sababu inaleta thawabu. Lakini thawabu hii ina maana tu pale ambapo Qur'ani inaathiri fikra na mawazo yetu. Bila athari hii, kuisoma mara elfu hakutakuwa na manufaa.”
Rais Pezeshkian aliwataka waelimishaji na viongozi kupandikiza uelewa wa kina wa Qur'ani miongoni mwa vijana, hasa wanafunzi. “Inatosha kuelewa undani wa jambo hili na kutambua kuwa Qur'ani ina nguvu ya kubadilisha na kuleta mapinduzi,” alisema.
Jumla ya watu 14 waliheshimiwa mwishoni mwa hafla hiyo kwa huduma zao kwa Qur'ani Tukufu. Hafla hiyo hufanyika kila mwaka katika mwezi wa Ramadhani.
4272447