Kwa mujibu wa shirika la habari la IQNA likinukuu tovuti rasmi ya Ofisi ya Rais, Rais Masoud Pezeshkian katika ujumbe wake huo amesisitiza kuwa:
“Idd al-Fitr ni dhihirisho la umoja na kuimarika kwa mafungamano ya kidini na kijamii miongoni mwa Waislamu, na ni wakati wa kupata matunda ya dua na ibada za dhati katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Natumai, kwa baraka na neema ya sikukuu hii iliyojaa rehema na baraka, tutaona mshikamano zaidi wa mataifa ya Kiislamu, kuimarika kwa amani na uthabiti kati ya nchi za Kiislamu, pamoja na kuongezeka kwa ushirikiano katika nyanja zote.”
Nchi kadhaa ulimwenguni kote zimetangaza rasmi kuwa Jumapili, Machi 30, 2025, ni siku ya kwanza ya Idul Fitr.
Katika eneo la Ghuba ya Uajemi, Saudi Arabia imetangaza Idul Fitr kuwa Jumapili kufuatia 'kuthibitishwa' kuonekana kwa mwezi mwandamo wa Shawwal katika Kituo cha Astronomia cha Tamir. Vivyo hivyo, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, na Kuwait pia zimethibitisha kuwa Idi itasherehekewa Jumapili baada ya kuthibitisha kuonekana kwa mwezi.
Wakati huo huo, nchi zingine zikiwemo Iran, Pakistan, Indonesia, Malaysia, Oman, Iraq, India, Syria, Brunei, Australia, Bangladesh, Morocco, Libya, Tunisia, Nigeria, Tanzania na Kenya zimethibitisha rasmi kuwa Jumapili itakuwa siku ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Mataifa haya yataadhimisha Idul Fitr kuanzia Jumatatu, Machi 31.
Idul Fitr ni sikukuu kubwa ya kidini inayosherehekewa na Waislamu duniani kote, yenye Swala ya Jamaa, sherehe, na utoaji wa msaada kwa wasiojiweza katika jamii ambao ni maarufu kama Zakatul Fitri.
4274353