Muungano huo umemaliza mkutano wake wa 19 mjini Jakarta kwa kutoa “Tamko la Jakarta,” likithibitisha tena msaada wake usiopingika kwa malengo ya ukombozi wa Palestina na kuitaka jamii ya kimataifa kuongeza shinikizo kwa utawala wa kikoloni wa Israel, ikiwemo vikwazo na kuutenga katika majukwaa ya dunia.
Tamko hilo, lililotangazwa na wajumbe wa mabunge kutoka nchi wanachama wa OIC, lilisisitiza “umuhimu wa kadhia Palestina na Al-Quds Al-Sharif (Jerusalem) kwa umma mzimaa Kiislamu,” likibainisha kuwa Mashariki mwa Al-Quds bado ni sehemu ya maeneo ya Palestina yaliyotekwa mwaka 1967 na ni mji mkuu halali wa taifa lijalo la Palestina.
Wajumbe walionyesha hofu kubwa kuhusu kuendelea kwa mashambulizi ya Israeli huko Gaza ambapo angalau watu 53,119, wengi wao wanawake na watoto, wameuawa tangu vita vya Israel kuanza Oktoba 2023.
Tamko pia limesisitiza ulazima wa kutekelelzwa agizo la muda la Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) lililotolewa Januari 26, 2024, pamoja na hati za kukamatwa zilizotolewa na Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Kimataifa (ICC) dhidi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa masuala ya kijeshi Yoav Gallant kwa makosa ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Tamko hilo lililaani mashambulizi “yasiyotofautishwa na yasiyokuwa ya uwiano” yaliyoendelea “bila kusitishwa.”
PUIC imetoa wito kwa “kusitishwa kabisa kwa mashambulizi ya Israeli yanayoendelea dhidi ya Palestina” na “kuachiliwa mara moja kwa wafungwa Wapalestina waliokamatwa kinyume cha sheria na kwa misukosuko na Israel, hasa wanawake na watoto.”
Pia lilikanusha mipango yoyote ya Israel ya kuunganisha sehemu za Gaza chini ya sababu za kuwatoa mateka au masuala ya usalama, na lilipinga vikali kuhamishwa kwa Wapalestina kutoka makazi yao.
Kwa wito wa moja kwa moja kwa jamii ya kimataifa, PUIC ilihimiza serikali kuweka vikwazo dhidi ya Israel, “kuzingatia maoni mawili ya ushauri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki,” na kuunga mkono uchunguzi unaoendelea wa ICC. Pia ilihimiza kuendelea kwa misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi za Wakimbizi (UNRWA).
3493108