IQNA

Jinai za Israel

Spika wa Bunge la Iran: Kinachotokea katika Ukanda wa Gaza leo ni aibu kwa ubinadamu

15:58 - January 10, 2024
Habari ID: 3478179
IQNA-Spika wa Bunge la Iran Mohammad Baqer Qalibaf anasema utawala wa Kizyauni wa Israel uliasisiwa kwa mauaji ya kimbari na vita na hivyo kuendelea kuwepo kwake kunategemea kutekeleza jinai hizo za kutisha.

Qalibaf aliyasema hayo Jumatano alipohutubia kikao cha 5 cha dharura cha wajumbe wa Muungano wa Mabunge ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (PUIC) katika mji mkuu wa Iran, Tehran.

Wakati wa mkutano huo, ulioitishwa chini ya anuanu ya:  "Ushirikiano wa Mabunge kwa ajili ya Palestina" na kuhudhuriwa na maafisa wakuu wa mabunge kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), wameshiriki ambapo wamejadili vita vya mauaji ya kimbari vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

Qalibaf alisema: "Kinachotokea katika Ukanda wa Gaza leo ni aibu kwa ubinadamu. Ni dhuluma maradufu kwa taifa ambalo limenyimwa haki zozote za binadamu na limekuwa chini ya hujuma na kukaliwa kimabavu kwa zaidi ya miongo saba.”

Halikadhalika amesema: "Hakuna dhamiri iliyoamka inayoweza kupuuza jinai za kutisha na za umwagaji damu zilizoenea zinazofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza na athari zake za kutisha kwa amani na usalama wa eneo na dunia."

Spika wa Bunge la Iran amesisitiza zaidi kuwa, kukaliwa kwa mabavu Palestina kwa muda wa miaka 75 na Israel na kuwatimua kwa nguvu wakazi wake wa asili katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza si suala linalohusiana na Wapalestina na utawala wa Israel pekee bali linahusu jambii ya mwanadamu na jumuiya ya kimataifa.

Spika wa Bunge la Iran aidha amekemea misimamo ya kindumakuwili ya nchi za Magharibi dhidi ya jinai za Israel huko Gaza na kusema: “Tunachoshuhudia Palestina siku hizi ni mfano wa wazi wa siasa za kinafiki na potofu za Marekani na washirika wake wa Magharibi katika kuunga mkono jinai hizo. umwagaji damu, utetezi kamili wa utawala dhalimu, na kukanusha kwa kina ukweli wa kihistoria na ustaarabu wa Palestina.

Pia ametaka kuundwa kwa kamati ya uchunguzi kuchunguza jinai za hivi punde za Israel huko Gaza na maeneo mengine ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu kwa ajili ya kuhukumiwa katika mahakama za kimataifa.

Spika wa Bunge pia alitoa wito wa kusitishwa mara moja vita vya utawala haramu wa Israel dhidi ya raia wa Palestina na utoaji wa huduma za kibinadamu kwa Gaza mapema iwezekanavyo.

3486760

Habari zinazohusiana
captcha