IQNA

Kadhia ya Palestina

Marekani, Utawala wa Kizayuni zinatekeleza Sera ya Njaa dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza

10:15 - June 20, 2024
Habari ID: 3478990
IQNA-Marekani na utawala wa Kizayuni zinatekeleza sera ya njaa katika Ukanda wa Gaza ili kuhakikisha Wapalestina wa eneo hilo wanaagamia kutokana na ukosefu wa chakul, maafisa katika eneo hilo la Palestina walisema.

 Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Serikali huko Ukanda wa Gaza, siku ya Jumanne iliulaumu utawala wa Israel na utawala wa Marekani kwa kutekeleza sera ya njaa dhidi ya watoto na wagonjwa wa eneo hilo la pwani.

Pia imeonya kuwa vikwazo vilivyowekwa na utawala katili wa Israel vinatishia moja kwa moja maisha ya Wapalestina milioni 2.4 katika ukanda huo uliozingirwa.

 Kwa mujibu wa ofisi hiyo, kwa sasa watoto elfu 3,500 wako katika hatari ya kifo kutokana na utapiamlo na ukosefu wa chanjo.

 Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Serikali ilisema utawala haramu wa Israel na Marekani lazima ziwajibike kwa matokeo ya uhalifu uliofanywa katika ukanda huo uliozingirwa.

 Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) lilisema katika taarifa yake siku ya Jumamosi kwamba zaidi ya watoto elfu 50,000 huko Ukanda wa Gaza wanahitaji matibabu ya haraka kwa utapiamlo uliokithiri.

 Shirika hilo lilionya kwamba "pamoja na vizuizi vinavyoendelea vya ufikiaji wa kibinadamu, watu huko Gaza wanaendelea kukabiliwa na njaa kali.

 Mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa wa (WHO) Aonya kuhusu ‘Njaa ya Janga’ huko Ukanda wa Gaza

"Timu za UNRWA zinafanya kazi bila kuchoka kufikisha huduma kwa familia kwa msaada, lakini hali bado ni mbaya.

 Utawala katili wa Israel umeweka vikwazo vikali kupeleka misaada ya kibinadamu, dawa na chakula kwa mamilioni ya watu huko Gaza tangu ilipoanzisha kampeni yake ya kijeshi yenye umwagaji mkubwa wa damu dhidi ya eneo lililozingirwa la Palestina Oktoba mwaka jana,2023.

 Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameuonya mara kadhaa utawala huo  haramu dhidi ya kutumia njaa kama silaha ya vita katika Ukanda wa Gaza.

 Zaidi ya watoto 16,000 wameuawa shahidi wakati wa uvamizi wa Israel tangu Oktoba, mwaka jana kulingana na makadirio ya hivi punde ya Wizara ya Afya ya Palestina na asilimia 98 ya watoto huko Ukanda wa Gaza hawana maji safi ya kunywa.

 

3488812

captcha