IQNA

Semina ya Al-Azhar yajadili uumbaji wa milima kwa mtazamo wa Qur’ani

21:49 - May 20, 2025
Habari ID: 3480712
IQNA – Semina kuhusu uumbaji wa milima kwa mtazamo wa Qur’ani ilifanyika katika Msikiti Mkuu wa Al-Azhar huko Cairo, Misri.  

Iliandaliwa Jumapili na kuhudhuriwa na wataalamu na watafiti wa miujiza ya Quran Tukufu.  

Wanazuoni wa Al-Azhar,  SheikhAbdul Fattah al-Awari na Sheikh Mustafa Ibrahim, walihutubia semina hiyo.  

Al-Awari alieleza kuwa milima ina uhusiano wa karibu na ardhi na ina jukumu muhimu katika kudumisha usawa na uthabiti wake.  

Aliongeza kuwa milima ni ishara ya nguvu za Mwenyezi Mungu na ushahidi wa uumbaji wake wa ajabu.  

"Hakuna mwanadamu yeyote, awe nani, anayeweza kuumba kazi ya sanaa kama hii. Jukumu la milima katika kuhifadhi usawa wa dunia litaendelea hadi Siku ya Kiyama."

Alirejelea Aya ya 105 ya Surah Taha:  

"(Muhammad),Na wanakuuliza khabari za milima. Waambie: Mola wangu Mlezi ataivuruga vuruga (Siku ya Kiyama).'"

Akifafanua, amesema kuwa Mwenyezi Mungu atang’oa milima na kuacha ardhi ikiwa tambarare bila kitu chochote juu yake Siku ya Kiyama.  

Akisisitiza umuhimu wa tafakuri ya kina juu ya aya za Qur’ani kuhusu milima, alisema kuwa tafakuri hii inadhihirisha ukubwa wa Muumba na nguvu zake za kushangaza katika kuumba ulimwengu.  

"Milima si ardhi tasa tu. Badala yake, ni ishara dhahiri na ushahidi thabiti wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu."

Mustafa Ibrahim alisema kuwa Qur’ani inarejelea milima kwa njia mbalimbali, ikitaja neno hilo mara 48 katika Surah tofauti.  

Alibainisha kuwa neno ‘milima’ inajitokeza kwa wingi mara 31 na kwa umoja mara 4 katika Quran.  

Aidha, alieleza kuwa Qur’ani haitumii tu neno “al-jibal” kuelezea milima, bali pia hutumia maneno mengine kama “al-rawasi”, ambalo linajitokeza mara 9 katika Quran, likionyesha uthabiti, nguvu, na jukumu lake katika kuimarisha ardhi.  

Alitaja Aya ya 79 ya Surah Al-Anbiya:  

Tuliifanya milima na ndege kumsifu Mola pamoja na Daudi."

Akifafanua, alisema kuwa aya hii inaonyesha kuwa viumbe hivi visivyo na uhai si vipofu au visivyo na hisia na utambuzi; bali ni viumbe vinavyomsifu Mola wao kwa namna ambayo Mwenyezi Mungu anajua vyema.  

3493154/

Habari zinazohusiana
Kishikizo: al azhar qurani tukufu
captcha