IQNA

Wenye vipaji vya Qur'ani katika Chuo cha Al Azhar waenziwa

11:00 - November 11, 2021
Habari ID: 3474540
TEHRAN (IQNA)- Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri amewaenzi na kuwatunuku zawadi wanafunzi walioshika nafasi za juu katika mashindano ya hivi karibu ya Qiraa ya Qur'ani Tukufu na Ibtihal.

Sherehe hiyo imefanyika Jumanne ambapo Sheikh Muhammad Zuwani, Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar amewaenzi wanafunzi waliofanikiwa.

Amesisitiza kuhusu azma ya Al Azhar ya kuunga mkono wenye vipaji vya Qur'ani na kuwaarifisha katika ulimwengu wa Kiislamu.

Wanafunzi kwa upande wao wamipongeza Al Azhar kwa kuandaa sherehe hizo na kusema hatua kama hizo zitaongeza motisha ya wanafunzi ili waweze kufanikiwa zaidi.

Chuo Kikuu cha Al Azhar ni chuo kikubwa zaidi cha Kiislamu duniani na kinafungamana na Msikiti wa Al Azhar. Chuo hicho kilianzishwa mwaka  364 Hijria Qamaria (975 Miladia) wakati wa Ukhalifa wa Fatimya kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu kwa wanafunzi wa maeneo yote ya dunia.

 

4012241

captcha