“Hakika nyumba ya kwanza [ya ibada] iliyowekwa kwa ajili ya wanadamu ni ile ya Bakka—iliyojaa baraka na ni mwongozo kwa walimwengu.” (Qur’ani 3:96)
Neno Bakka linamaanisha mahali pa msongamano, ardhi tukufu ambako vizazi vya waumini wamekusanyika kwa ibada kwa karne nyingi. Ndani ya mahali hapa, baraka, neema ya Mungu na faida ya kudumu, inaendelea kutiririka.
Miongoni mwa pingamizi zilizotolewa na Bani Isra’il ilikuwa uelekezaji wa Qibla kutoka Al-Quds (Jurusalem) kwenda Kaaba, mjini Makka. Wengine walijiuliza kwa nini Waislamu wamechagua nyumba hii ya kale, licha ya historia ya Al Quds na ujenzi wake wa mahali patakatifu na Nabii Sulayman (AS). Qur’ani inajibu kwa hakika kwamba Kaaba inashika nafasi ya kwanza kama Nyumba asili ya ibada, ikitangulia kwa umri na maelekezo ya kimungu.
Aidha, Mwenyezi Mungu (SWT) anaangazia alama dhahiri zinazothibitisha tauhidi ndani ya mahali hapa patakatifu. Maqam Ibrahim, mahali ambapo Nabii Ibrahim (AS) alisimama alipokuwa akijenga Kaaba, bado unasalia kama ushuhuda wa ibada na unyenyekevu.
Qur’ani inaelezea Kaaba kwa maneno mbalimbali, ikionyesha nafasi yake kama:
Msingi wa utulivu kwa wanadamu (Qur’ani 5:97)
Nyumba huru na isiyo na umiliki wa kibinadamu (Qur’ani 22:29)
Mahali pa mkusanyiko na makazi salama kwa watu (Qur’ani 2:125)
Katika aya inayojadiliwa (Qur’ani 3:97), usalama umetajwa kama sifa muhimu ya ardhi hii. Kaaba inasimama kama kimbilio la milele kwa nyoyo zinazotamani ukaribu na Mola, ambako waumini wanatafuta faraja chini ya kivuli cha rehema za Mwenyezi Mungu.
3493332/