IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Makkah: Roboti Zatumika Kuboresha Huduma kwa Wageni

23:59 - August 11, 2025
Habari ID: 3481072
IQNA – Roboti za kielektroniki zinazoweza kuingiliana na watumiaji zimetumika katika toleo la 45 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani yanayofanyika Makkah kwa lengo la kuboresha huduma kwa wageni.

Mradi huu unaoendeshwa kwa teknolojia unasaidia kuwapa washiriki na wageni ufikivu wa haraka kwa taarifa na mwongozo kwa njia ya kisasa na rahisi kutumia.

Roboti hizi zikiwa na skrini za kugusa zinazowezesha mawasiliano, zinatoa maelezo kamili kuhusu mashindano, yakiwemo ratiba za matukio, maeneo ya kufanyia mashindano, na mwongozo wa ushiriki.

Aidha, zina uwezo wa kujibu maswali kwa lugha 96, jambo linalowezesha hafla hii kuwahudumia watu kutoka mataifa na asili mbalimbali.

/3494201

captcha