IQNA

Washindi wa Mashindano ya Afrika ya Kuhifadhi Qur’ani na Hadithi Watunukiwa Johannesburg

18:08 - September 23, 2025
Habari ID: 3481271
IQNA – Hatua ya mwisho ya Mashindano ya Mfalme Salman bin Abdulaziz ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtume (SAW) barani Afrika imehitimishwa kwa hafla rasmi iliyofanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Hafla ya kufunga mashindano hayo ilifanyika Jumamosi jioni kwa mpango wa Wizara ya Mambo ya Kiislamu, Da’wah na Mwongozo ya Saudi Arabia, katika Ukumbi wa Mikutano wa Sanduto, Johannesburg.

Viongozi wa ngazi za juu, mabalozi wa mataifa mbalimbali, wanadiplomasia, na wawakilishi wa taasisi za Kiislamu walihudhuria hafla hiyo. Tukio hilo liliripotiwa kwa upana na vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa.

Waziri wa Mambo ya Kiislamu wa Saudi Arabia, Sheikh Abdullatif bin Abdulaziz Al-Sheikh, kupitia hotuba iliyowasilishwa kwa niaba yake na Naibu Waziri Awad bin Sabti Al-Anzi, alieleza kuwa nchi yake huandaa mashindano ya kuhifadhi Qur’ani kimataifa na kitaifa, na imeanzisha Kituo cha Mfalme Fahd cha kuchapisha Qur’ani kwa lengo la kuitafsiri kwa lugha mbalimbali.

Akisisitiza kuwa Qur’ani Tukufu ndiyo chanzo cha heshima na fahari ya taifa, aliwahimiza washiriki kushikamana na Qur’ani, kuishi kwa mujibu wa mafundisho yake, na kuielewa kwa usahihi bila kupotoka au kuwa na misimamo mikali.

Hatua ya mwisho ya mashindano hayo ilianza Alhamisi, ikiwajumuisha washiriki 44 kutoka nchi 29. Washiriki 12 walitangazwa kuwa washindi wa juu, ambapo 9 walikuwa katika fani ya kuhifadhi Qur’ani, na 3 walitambuliwa kwa umahiri wao katika kuhifadhi Hadithi za Mtume (SAW).

Jumla ya zawadi zilizotolewa katika mashindano haya zilikuwa Riyali 300,000 za Saudi Arabia, ambazo ziligawiwa kwa washindi wa juu katika fani mbalimbali wakati wa hafla ya kufunga mashindano.

3494709

captcha