IQNA

Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani kuundwa

19:22 - November 04, 2025
Habari ID: 3481463
IQNA – Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu na Mahusiano ya Kimataifa amesema kuwa taasisi hiyo inapanga kuanzisha Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu.

“Tunajitahidi kwa uwezo wetu wote kuwasilisha sura halisi na inayostahiki ya Iran kwa mataifa ya nje. Kuna shughuli nyingi na za aina mbalimbali katika juhudi hizi. Kwa hivyo, tutazindua Taasisi ya Kimataifa ya Qur’ani chini ya usimamizi wa Ustadh Hamed Shakernejad, msomaji mashuhuri wa kimataifa wa Qur’ani na balozi wa Qur’ani wa Iran,” alisema Hujjatul-Islam Mohammad Mehdi Imanipour katika kikao cha tatu cha waratibu wa swala kilichoandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu.

“Dhamira ya taasisi hii ni kutekeleza shughuli za Qur’ani kwa upana na kwa ustadi,” alisisitiza.

Aidha, alizungumzia umuhimu wa kueneza swala katika jamii, akisema: “Ni wajibu wetu sote kusimama kwa pamoja kutekeleza jukumu hili tukufu.”

Aliongeza kuwa miongoni mwa haki za swala ni kuiswali kwa jamaa. “Tuipe swala heshima yake ili nasi tuheshimiwe katika Akhera. Hatua ya kwanza ya kuiheshimu ni kuiswali kwa jamaa, na kuiswali kwa wakati wake sahihi , mara tu baada ya adhana, ni jambo la msingi.”

Mwanazuoni huyo amesisitiza kuwa ni lazima swala za jamaa ziswaliwe katika taasisi zote, na juhudi zifanywe kuhakikisha mazingira ya vyumba vya swala yanapendeza, safi, na yanavutia.

Hujjatul-Islam Imanipour alihimiza umuhimu wa kuendeleza swala za jamaa katika vituo vya kiutawala, na akasema kuwa ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mikutano ya kitaifa ya Makao Makuu ya Swala ni hazina ya kusomwa, yenye hekima kubwa katika kuendeleza malengo ya baadaye na sera, na ni lazima tuyazingatie kwa uzito mkubwa.

3495245

Habari zinazohusiana
captcha