Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Kueneza Qur'ani na Uenezi cha Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu (ICRO) Hujjatul Islam Seyed Mostafa Hosseini Neyshabouri ameyasema hayo alipotembelea Chuo Kikuu cha Sayansi ya Qur'ani mjini Jakarta, Indonesia.
Amesema Qur'ani inatoa wito wa kuanzishwa uhusiano baina ya dini za Tauhidi ili kuzuia mifarakano.
Qur'ani Tukufu inatanguliza imani ya Mungu mmoja kama nguzo ya umoja wa kimataifa, amesema.
Kwingineko katika matamshi yake, Hujjatul Islam Hosseini Neyshabouri alisisitiza haja ya kusoma na kuendeleza diplomasia ya Qur'ani.
Katika dunia ya leo, ambayo inakabiliwa na migogoro mbalimbali ya kijamii, kisiasa, kijeshi na kiutamaduni, diplomasia ya Qur'ani inayounganisha inaweza kufanya sauti ya Qur'ani Tukufu isikike katika ulimwengu wa Kiislamu na miongoni mwa wanadamu kwa ujumla.
Sababu ya kuwa na uadui na Uislamu na Qur'ani ni kwamba madola yenye kiburi yanaogopa kuenea kwa harakati ya Qur'ani na yanaonyesha hofu yao kwa njia ya chuki ya Uislamu, aliendelea kusema.
Afisa huyo wa ICRO pia alisema kwa kuzingatia ulazima wa mafunzo ya Qur'ani na kufikisha thamani za Qur'ani kwa vizazi vijavyo, kuwekeza katika nyanja ya elimu ni jambo la lazima.
Katika ziara hiyo, Najma al-Faeza, rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Qur'ani mjini Jakarta, alitoa wito wa kuimarishwa uhusiano wa Qur'ani kati ya Iran na Indonesia.
Pande hizo mbili pia zilijadili kutumia uwezo wa kielimu wa nchi hizo mbili kuimarisha shughuli za Qur'ani.
3490455